Mfano wa Kuigwa!! FAMILIA YATOA ZAWADI YA PASAKA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI NA KAMBI YA WAZEE SHINYANGA

Ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhanghija jumuishi kilichopo mjini Shinyanga,ambapo familia ya bi na bwana Mwalongo ya Mjini Shinyanga ambayo jana imetoa msaada wa chakula kwa watoto hao kwa ajili ya kufurahi nao kusherehekea sikukuu ya pasaka katika kuonesha upendo kwa watoto hao,ambao inadaiwa wazazi wamewatelekeza kiasi cha kutowatembelea pindi wanapowapeleka katika kituo hicho


Kushoto ni mwalimu mlezi wa kituo cha Buhangija jumuishi bi Maisala Adinani akipokea msaada wa chakula ambacho ni  unga wa sembe kilo hamsini , mchele kilo 50 pamoja na Mafuta ya kupikia Lita kumi,kulia ni bwana Josephat Mwalongo akiwa na mke wake Anna Mwalongo wakikabidhi chakula

Kushoto ni  mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Hassan Hamis akiwakilisha watoto wenzake akipokea zawadi ya mbuzi wawili(mmoja hayupo pichani) kutoka familia ya Mwalongo

Ni katika kambi ya kulelea wazee wasiojiweza Kolandoto mjini Shinyanga ambako pia familia ya Mwalongo ilitoa zawadi ya pasaka kwa wazee hao mbuzi wawili,unga wa sembe kilo hamsini,mchele kilo hamsini na mafuta ya kupikia lita kumi kulia aliye simama ni msaidizi wa Afisa Ustawi wa jamii katika kambi hiyo bi Evodia Ndaka

Kushoto ni mzee Samwel Maganga mwenyekiti wa kambi ya wazee Kolandoto akipokea mbuzi kutoka katika familia ya Mwalongo ya mjini Shinyanga-PICHA ZOTE KWA HISANI YA MARCO MADUHU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post