MFAHAMU HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE

HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE

Edward Moringe Sokoine alizaliwa tarehe 1 Agosti 1938 alikuwa Waziri  Mkuu wa Tanzania tarehe 13 Februari 1977 hadi tarehe 7 Novemba 1980 tena akawa Waziri mkuu toka tarehe 24 February hadi tarehe 12 Aprili 1984.

Alikuwa ni mtu aliyepanda usawa kwa kila mtu aliamini
kila mtu anaweza kuwa na maendeleo kama akijituma katika kilimo na sehemu alipo pamoja na kujitegemea akiwa ni wakala wa 
mabadiliko katika nchi, mtu asielaumu na mwaminifu.

Alizaliwa Monduli Mkoani Arusha Tanzania,  alipata elimu 
ya msingi na sekondari katika miji ya Monduli na Umbwe toka mwaka
1948 hadi 1958.

Mwaka 1961 alijiunga na chama cha TANU  baada ya kuchukua masomo katika Uongozi nchini Ujerumani 1962 hadi mwaka 1963.

Aliporudi kutoka Ujerumani alikuwa Afisa Mtendaji 
wa Wilaya ya Masai, tena akachaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo 
la Masai.

Mwaka 1967 alikuwa naibu waziri wa mawasiliano, usafirina kazi.

Hatua nyingine katika maisha yake alijitangaza mpaka kuwa Waziri Mkuu 1970.

Mwaka 1972 aliamia kwenye Waziri wa usalama na Mwaka 1975 
alichaguliwa kwenye Bunge tena wakati huu kupitia Monduli.

Miaka miwili baadae akawa mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), 1977 alianza muhula wa kwanza ofisini akiwa 
Waziri Mkuu wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania.

Muhula huu  ulidumu hadi 1981, baada ya kutulia kwa kipindi cha mwaka alikuwa  tena Waziri Mkuu tena mwaka 1983, alikaa mwaka mmoja ofisini mpaka alipofariki Aprili 1984 kwa ajali ya gari.

Kuhusu chuo cha Sokoine Kuna Chuo Morogoro Tanzania kinaitwa jina lake (Sokoine University Of Agriculture (SUA) chuo hiki kilianza mwaka 1984 kama chuo cha kilimo kinachotoa diploma katika kilimo.

Chuo hicho kikaongezwa hadi kutoa mchepuo wa
kilimo mwaka 1969 chini ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.

MAKALA FUPI YA SOKOINE:

“Tulimlazimisha kuwa msaidizi wa chifu Mkuu wa Council ya Maasai land akimsaidia Chifu Barnoti na ilipofika kipindi cha uchaguzi wa mbunge tukamlazimisha kuchukua fomu kuchuana na mzee Barnoti, tulifanya kampeni ya chini chini hadi akashinda,” anasimulia.

“Tutakutana tena kwa kikao kijacho cha Bunge hapa Dodoma. Mimi ninasafiri kwa gari kwenda Dar es Salaam, nitapitia Morogoro, naamini tutaonana huko.” Edward Sokoine. 

MATUKIO KATIKA PICHA:
Msimamizi wa eneo hilo, Hamis Said Mpandachuri kulia akiwa na mwandishi wa Mwananchi Morogoro, Venance George. 

Mifugo ikipita eneo hilo na kuchafua mazingira


Sehemu ambayo gari la Sokoine lilianguka chini baada ya kupata ajali kando ya barabara kuu ya Dodoma-Morogoro eneo la Wami-Dakawa.
JINSI AJALI ILIVYOKUWA

Ilikuwa Jumatano ya Aprili 12, 1984 saa 11:30 jioni, siku ambayo Dar es Salaam ilinyesha mvua kutwa nzima. 

Wakati kipindi cha salaam cha Jioni Njema cha Redio Tanzania (RTD) wakati huo kikiwa hewani, mara matangazo yake yanakatishwa ghafla na wimbo wa taifa unapigwa.

Mara inasikika sauti iliyozoeleka ya Rais Nyerere wakati huo ikisema: 

“Ndugu wananchi, leo majira ya saa 10 jioni, ndugu yetu, kijana wetu na mwenzetu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine wakati akitoka Dodoma kuja Dar es Salaam, gari yake imepata ajali, amefariki dunia.”

Takribani miaka 29 imepita tangu kufariki kwa, Edward Moringe Sokoine, aliyepata kuwa waziri mkuu wa Tanzania katika vipindi viwili tofauti kabla ya kufariki Aprili 12, 1984.

Sokoine alikufa baada ya kutokea ajali ya gari eneo la Wami-Dakawa, wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea mjini Dodoma alikokuwa akishiriki vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

KUMBUKUMBU YA KILA MWAKA:

Aprili 12 ya kila mwaka, taifa limekuwa likiadhimisha kumbukumbu ya kiongozi huyo kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kuendesha makongamano, midahalo, mabonanza, ibada, riadha na upandaji mlima Kilimanjaro.

Katika utawala wa hayati baba wa taifa na rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika eneo la Wami  Sokoine kulijengwa nyumba moja na banda moja linalotumika kama jukwaa lakini kwa sasa majengo hayo yamechakaa, anasema msimamizi wa eneo hilo, Hamis Said Mpandachuri.

Waandishi walifika katika eneo hilo na kukuta mnara wa picha ya Sokoine ukiwa umepakwa rangi mpya za manjano, kijani, blue na nyeusi huku chini ya picha yake kukiwa na maneno “Alimtumikia Mungu kwa kuwatumikia watu, sauti ya watu ni sauti ya Mungu”.

Mbali ya mnara huo na majengo yaliyojengwa katika utawala wa serikali ya kwanza, pia liko jengo jipya na la kisasa ambalo linaendelea kujengwa nyuma ya majengo ya zamani. 

Kwa mujibu wa uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero, jengo hilo ni kwa ajili ya shule ya sekondari ya Sokoine (Sokoine memorial high school), inajengwa kama sehemu ya jitihada za wilaya hiyo za kumuenzi Sokoine.

Mbali na jitihada za halmashauri hiyo, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ambacho pia kimebeba jina lake kimekuwa katika mikakati ya kuhakikisha kuwa kinamuenzi kiongozi huyo kwa kila hali. 

Kassim Msagati ni ofisa mawasiliano wa chuo hicho,  anasema hayati, Edward Moringe Sokoine, alikuwa muhimili muhimu wa kuanzishwa wa chuo kikuu hicho cha kilimo ambacho ni chuo kikuu pekee cha kilimo cha Serikali nchini.

Aprili 12, 1984 bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo hayati Sokoine alishiriki lilipitisha sheria namba 6 ya mwaka 1984 ya kuanzishwa kwa chuo kikuu cha kilimo Morogoro. 

Hapo kabla chuo hicho kilikuwa ni kitivo cha kilimo cha kilimo na misitu cha chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Msagati, sheria hiyo iliyopitishwa na bunge ilikiidhinisha kitivo cha kilimo cha chuo kikuu cha Dar es salaam kilichokuwa Morogoro kuwa chuo kikuu na kutaka kiitwe chuo kikuu cha kilimo Morogoro.

Lakini chuo hicho kililazimika kubadilishwa jina hata kabla ya jina la awali kuanza kutumika na kuitwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA). 

Hii ilitokana na kifo cha kiongozi huyo, muda mfupi baada ya chuo hicho kuidhinishwa rasmi kwa sheria hiyo ambapo utekelezaji wake ulipaswa kuanza mwezi Julai, 1984, ndipo serikali ikakubali kiitwe Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post