Makubwa haya!! MSICHANA AISHI NA TUMBILI CHUMBA KIMOJA KWA MIAKA 9

xx
Polisi nchini Argentina wamemwokoa msichana mwenye umri wa miaka kumi na tano ambaye alifungiwa katika chumba cha kuegesha magari na kunyimwa chakula pamoja na kupigwa na wazazi waliokuwa wakimlea kwa kipindi cha miaka tisa.


Msichana huyo aliishi na Tumbili kwenye chumba cha kuegeshea magari ambapo baada ya kupimwa alikutwa na uzito wa kilo ishirini na kusema alikuwa akipigwa kila mara iwapo angejaribu kula mabaki ya chakula kilichotupwa kwa wanyama hao.
Alifanikiwa kuondoka katika eneo hilo la kuegesha magari mara mbili tu katika kipindi cha miaka yote tisa,walezi wake wamekamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kumfanya kama mtumwa.
Msichana huyo kwa sasa amelazwa hospitlaini alipatikana na dadake wa kuzaliwa naye mjini Buenos Aires kwa mujibu wa maafisa wakuu,wazazi wake waliamriwa na Mahakama kumkabidhi kwa walezi mwaka 2001 baada ya wazazi wake wa kumzaa kukosa uwezo wa kifedha wa kumlea.
via< bbc.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post