KUHUSU AJALI YA BASI LA SUMRY KUUA WATU 19 HUKO SINGIDA

 Basi la kampuni ya Sumry lenye namba za usajili, T 799 BET lililouwa watu 18 mkoani Singida.
 Gari la polisi likiwa limepakia maiti zaidi ya kumi zikipelekwa hospitali ya mkoa wa Singida kwa ajili ya kuhifadhiwa na kutambuliwa.…
Basi la kampuni ya Sumry lenye namba za usajili, T 799 BET lililouwa watu 18 mkoani Singida.
Gari la polisi likiwa limepakia maiti zaidi ya kumi zikipelekwa hospitali ya mkoa wa Singida kwa ajili ya kuhifadhiwa na kutambuliwa.
Moja ya maiti ya ajali ya basi la Sumry iliyotokea katika kijiji cha Utaho, Wilayani Ikungi mkoani Singida ikisubiri kupakiwa katika gari la polisi.

Watu 19 wa kijiji cha Utaho, wilayani Ikungi mkoani Singida wamepoteza maisha wakiwemo askari wanne wa jeshi la polisi, baada ya kugongwa na basi la Summry wakati wakiwa wanatoa msaada wa kumpakia marehemu kwenye gari la polisi aliyegongwa na gari kubwa ambalo halikufahamika mara moja jana usiku.

Basi hilo la kampuni ya Sumry hufanya safari zake kati ya Kigoma na Dar-es-Salaam.

Taarifa zinasema Dereva wa basi hilo alikimbia mara tu na baada ya ajali hiyo na kulitekeleza basi hilo.

Mwandishi wa habari Elisante Mkumbo alifika na kuwakuta wasafiri walionusurika wakiwa  katika kituo cha polisi cha Ikungi bila ya kujua hatima yao ya  safari baada ya basi lao kuwakanyaga na kuuwa watu 19.

Picha zote kwa hisani ya Elisante Mkumbo-ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post