Kizaa zaa!! MWANAFUNZI AVAMIA SHULE AKIWA NA PANGA,UPINDE,MISHALE NA RUNGU,WALIMU WATOKA NDUKI

Walimu na wanafunzi wa Sekondari ya Kambarage wilayani Serengeti wamejikuta katika wakati mgumu kutokana na mmoja wa wanafunzi kuvamia shule akiwa na silaha za jadi akitishia kuwadhuru huku ikidaiwa kuwa alikumbwa na pepo.
Katika tukio hilo inadaiwa wanafunzi wawili wa kike walipoteza fahamu kwa hofu. Tukio hilo linadaiwa kutokea Aprili 23 saa 6:00 mchana na kudumu kwa zaidi ya dakika 25.
Makamu Mkuu wa Shule, Charles Malima alisema akiwa ofisini ghafla alisikia kelele za walimu wa kike waliokuwa wakisubiri usafiri wakiomba msaada wakiwa wanakimbia huku mwanafunzi akiwafukuza akiwa ameshika panga.
“Nilidhani wameumwa na nyuki walioko eneo hilo… Nilipoangalia nikamwona mtu ameshika panga, upinde, mishale miwili na rungu kiunoni akiwafukuza kwa kasi, wananchi walikuwa nyuma wanakuja kuwaokoa,” alisema Mwalimu Malima.
Na Anthony Mayunga, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post