WACHIMBAJI WA MADINI WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WATATU KUJERUHIWA BAADA YA KUPONDWA NA UDONGO

Watu wawili wamekufa na watatu kuokolewa katika machimbo ya wachimbaji wadogowadogo mchanga yaliyoko katika kijiji cha Mponvu wilayani Geita baada ya  kufukiwa na udongo ndani ya shimo.

Tukio hilo limetokea Machi 9 mwaka huu majira saa 6 usiku ambapo watu watano walipanda katika mlima wa Samina na kuanza kuchimba mara ghafla udongo uliporomoka na kuwaponda waliokuwemo ndani ya shimo hilo.

Waliopondwa  na udongo ni  Ngambi Makula(32) mkazi wa Nyarugusu,Juma Makoye(36) mkazi wa Bomani na waliookolewa ni Mabela Maduhu(31) mkazi wa Mpomvu,Harji Zacharia(26) mkazi wa Nyarugusu,Salama Magangu (26) mkazi wa Busanda.

Mganga wa zamu wa hospitali ya wilaya ya Geita Dk,George Rweyemela amethibitisha kupokea miili miwili ya marehemu na majeruhi watatu ambao wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku miili ya marehemu iliyokuwa imehifadhiwa chumba cha maiti imeshatambuliwa na ndugu zao na wameshaichukua kwa mazishi.

Kamanda wa polisi mkoani hapa kamishina msaidizi mwandamizi Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa hakuna mtu aliyekamatwa na  amewaasa vijana kutoenda maeneo hatari ambayo yanaweza kusababisha maafa wakati taifa bado linawahitaji kulitumikia,alisema kamanda huyo kwa uchungu wa tukio hilo.
 
Tukio hili limetokea siku chache tu baada ya watu wawili  kukaa ndani ya shimo kwa siku 4 kisha kuokolewa  wakiwa hai katika machimbo ya mgodi wa GGM eneo la Kukuluma mkoani Geita.
Na Valence Robert-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post