Updates!!! FREEMASONS WAHUSISHWA,KIFO CHA MTOTO ALIYEKATWA KOROMEO NA BABA YAKE HUKO KAHAMA


Mtoto Said Joshua enzi za uhai wake akiwa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kabla ya kupelekwa Bugando jijini Mwanza baada ya kukatwa koromeo na Baba yake


Huzuni kubwa imetanda baada ya mtoto Said Joshua (12) aliyekatwa koromeo  kwa kutumia kisu na baba yake aitwaye Joshua Salvatory (37),usiku wa kuamkia tarehe 4 mwezi huu katika kitongoji cha Majengo Kaskazini,kata ya Majengo,wilayani Kahama mkoani Shinyanga ,kufariki dunia jana jioni wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo Kaskazini Noel Makula Museven ameimbia www.malunde1.blogspot.com kuwa mtoto huyo alifariki dunia akiwa Bugando alikokuwa amelazwa kwa matibabu zaidi mara baada ya hali yake kuwa mbaya katika hospitali ya wilaya ya Kahama alikokuwa anapatiwa kutokana na koromeo lake kukatwa lote kwa kisu na baba yake kutokana na kile kilichodaiwa kuchoka kumtibu maradhi yaliyokuwa yanamsumbua mara kwa mara. 

Kitendo cha kuchinjwa kwa mtoto Said Joshua na hatimaye kusababisha kifo chake kimeibua mambo mengi huku baadhi ya wakazi wa Kahama wakidai kuwa pengine kitendo hicho kinatokana na imani za kishirikina kwa madai kuwa mtuhumiwa alikuwa amemtoa sadaka mwanae kwa waganga ili kupata utajiri na kwamba Salvatory amefanya kitendo hicho kwa lengo la kulipa mchango wa Freemason huku wengine wakidai kuwa alitaka kuchangia damu ya mtoto mdogo akakataliwa.

“Katika miaka kama minne/mitano iliyopita mtuhumiwa alikuwa tajiri,na utajiri huo inasemekana ulitokana na kumtoa ndagu mtoto wake,akaharibu akili ya mtoto,kila mwezi mtoto akawa anaanguka kifafa, inasemekana  alikiuka masharti ya mganga wake pesa zikamwishia na mtoto wake akaendelea kubaki katika hali ya kuugua mara kwa mara ikiwemo kuanguka kifafa kila mwezi”alisema Museven

Mwenyekiti huyo wakitongoji amefafanua kuwa kabla ya kumkata koromeo mwanaye pia mwezi Julai mwaka jana Salvatory alitaka kumchinja mke wake Mariam Idd lakini yeye (Museven) akawasuruhisha na mke wa mtuhumiwa kuamua kumkimbia mme wake kwa hofu ya kuuawa na mwanamme kubaki na mtoto Said Joshua.

 “Siku chache tu baada ya kuwasuruhisha Salvatory alitaka kumchinja pia  mtoto wa jirani yake kwa madai ya kwanini huwa anacheza na mwanaye ,nikaingilia kati kitendo hicho kilimuudhi Salvatory na kutaka kunichinja pia,nikaita polisi akakamatwa,na ndiyo tuhuma iliyompeleka gerezani kwa kipindi cha miezi miwili,”,alieeleza Museven.

Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo Mariamu Idd (35) alisema, mtoto wake alichukuliwa na baba yake mzazi siku moja kabla ya tukio na  kwenda naye kwake mitaa ya Majengo kwa kuwa  alikwisha achana na mwanamme huyo siku nyingi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa  polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla kwa vyombo vya habari ya tarehe 5,mwezi Machi 2014,alisema chanzo cha tukio hilo inasadikiwa chanzo cha tukio hilo kinasaikiwa kuwa mtuhumiwa anaugua ugonjwa wa akili.

Akizungumza na www.malunde1. blogspot.com mapema leo kamanda Mangalla amesema kinachofuatia sasa ni mtuhumiwa kufikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma za mauaji zinazomkabili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post