Ukatili wa kutisha Geita!!! MWANAMKE AUAWA BAADA YA KUGOMA KULALA NA MKE MWENZA CHUMBA KIMOJA,MWANAMME ALITAKA AFANYE NAO TENDO TAKATIFU KWENYE CHUMBA KIMOJA

 
Siku chache tu baada ya dunia kuadhimisha siku ya wanawake,lakini wakati huo wanaharakati wa haki za binadamu,ikiwemo TAMWA kuendelea kupiga vita ukatili wa kijinsia,Mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina la Constancia John (28) Mkazi wa kijiji cha Ichwankima wilayani Chato mkoani Geita,  amefariki dunia baada ya kupigwa na mume wake Joseph Clemence(34) kwa tuhuma ya kumnyima tendo la ndoa baada ya kumlazimisha mwanamke huyo alale chumba kimoja na mke mwenzie.
 
Tukio hilo limetokea majira ya saa sita usiku wa kuamkia jana baada ya Clemence kumpiga mkewe Constancia na kumburuza kutoka nje hadi kumuingiza ndani, na kutokana na kipigo hicho mwanamke huyo akapoteza maisha.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo cha mgogoro huo ni Clemence ambaye  ana wake wawili kuwalazimisha kulala nao chumba kimoja kwa ajili ya tendo la ndoa, jambo ambalo Constancia alilikataa na kusababisha ugomvi huo

Kamanda wa polisi mkoani Geita kamishina msaidizi mwandamizi Leonard Paul  amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Kufuatia tukio hilo katibu wa kituo cha sheria na haki za binadamu wilayani Geita Elineema Charles ametaka hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi ya Clemence, na kuwa fundisho kwa wengine kwani kitendo hicho hakivumiliki katika jamii.

Na valence Robert-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post