Siasa bwana!!! DIWANI WA CCM AKAMATWA NA KADI FEKI KIBAO ZA CHADEMA,ZINA SAINI YA MBOWE

Kadi feki za CHADEMA alizokutwa nazo
Diwani wa viti maalumu wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kalangalala na tarafa ya Geita wilayani Geita mkoani Geita Zaitun Sued Fundikira  anayeishi katika mtaa wa Mission .
Kadi feki za CHADEMA zikiwa na saini ya mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe


Diwani wa viti maalumu wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kalangalala na tarafa ya Geita wilayani Geita mkoani Geita Zaitun Sued Fundikira  anayeishi katika mtaa wa Mission amekamatwa na kadi za kugushi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).Kadi zilizogushiwa ni 23 zikiwa na saini ya mwenyekiti CHADEMA taifa Freeman Mbowe,kadi ambazo hazijaandikwa chochote katika baadhi ya sehemu kama vile jina la mwanachama na sehemu anayokaa.Wakisimulia juu ya tukio hilo mashuhuda walisema kuwa mnamo saa nne asubuhi alitokea mtoto mmoja akiwa na kadi za Chadema amezishika mkononi akitembea nazo mtaani na kutokeza katika kijiwe cha Kalakana ya wakereketwa wa Chadema maarufu kama “Kijiwe cha Sengerema” ndipo walipomuona mtoto huyo walipomuuliza akasema kuwa amezitoa ndani kwani zimo nyingi sana.Mara baada ya kuambiwa hivyo wakamwambia mtoto huyo awapeleke na mtoto huyo aliongozana nao hadi nyumbani kwa diwani huyo na walipofika ,mtoto aliingia ndani na kuwaletea kadi nyingi mkononi huku akiwa na mkoba umejaa kadi zingine.Muda mchache tu baada ya mtoto kutoka na kadi hizo huku wakereketwa hao wakizichukua ghafla diwani huyo alijitokeza nje huku akihaha na kufoka kuwa hizo kadi hazijui. “Nashangaa mimi kadi hizi sizijui kabisa licha ya kuwa kwenye mkoba wangu lakini sijui nani aliyeziweka humu,na mwandishi yeyote atakayeniandika nitamshtaki’’,alieeleza diwani huyo.Taarifa za kuaminika kutoka kwa wananchi wamesema kuwa diwani huyu amekuwa akiratibu shughuli mbalimbali za kutaka kudhoofisha Chadema katika eneo hilo ambapo inadaiwa kuwa hadi kombati za Chadema zimeshaandaliwa ikiwa ni pamoja na kadi hizo feki kwa ajli ya kuhakikisha ujio wa aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe atakapokuja kanda ziwa wapewe watu kadi hizo na kuvulishwa kombati za chama ili watamke kuwa wamejitoa Chadema.Mwenyekiti wa mtaa wa mission  anakoishi diwani huyo wa viti maalum,Juma Kajala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.Baadhi ya watu wamesema kuwa diwani huyo amekuwa akiratibu mambo mengi lakini cha ajabu wamemshangaa kugushi hadi sahihi za mwenyekiti wa CHADEMA taifa wakati mwenyekiti taifa hagawi kadi .Uchunguzi umebaini kuwa hata ndani ya chama cha mapinduzi mtoa taarifa amesema kuwa diwani huyo aliwahi kuteuliwa kuwa katibu wa jumuiya ya wanawake wilayani Geita lakini baadae uteuzi wake ulisitishwa mara moja baada ya kubaini kuwa mienendo yake siyo mizuri hivyo hadi CCM walishamshtukia.Naye kaimu katibu wa mkoa wa Chadema Rogers Luhega alisema kuwa wa tayari taarifa hizo wameshazipeleka katika kituo cha polisi Geita na kufungua jalada  la mashitaka kwa ajili ya kumshitaki diwani huyo.Na Valence Robert- Geita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post