Sakata la Ushoga!!! UGANDA YAITUHUMU BENKI KUU YA DUNIA KWA USALITI

Msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono OpondoMsemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo 

Serikali ya Uganda imeituhumu Benki ya dunia kwa usaliti, baada ya Taasisi hiyo ya fedha duniani kusitisha mkopo wa dola milioni 90 kwa nchi ya Uganda kufuatia nchi hiyo kupitisha sheria kali dhidi ya ushoga.

Msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo amesema kupitia kwenye mtandao wa twiter, kwamba benki ya dunia ni taasisi ya mataifa mbalimbali hivyo haipaswi kuwasaliti wanachama wake hata kama ni wadogo kiasi gani.

Siku ya Alhamisi Benki ya Dunia ilitangaza kusitisha mkopo wa dola milioni 90 uliolenga kuisaidia nchi ya Uganda kuimarisha mfumo wake wa afya baada ya Rais Yoweri Museveni kusaini sheria kali ya kupinga vitendo vya ushoga nchini Uganda.

Hata hivyo Uganda imesema haitatishika na vitisho vya mataifa ya Magharibi kuhusu kusitisha misaada yake nchini humo kufuatia kupitishwa kwa sheria hiyo.
via_rfi kiswahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post