Katika hali isiyokuwa ya kawaida wachimbaji wadogo kwenye machimbo ya
Mwashina wilayani Nzega mkoani Tabora wametakiwa kuondoka eneo hilo kuanazia
leo.Habari kutoka katika machimbo hayo zinasema kuwa tayari askari
polisi wapo eneo hilo hata hivyo wachimbaji hao wanasema kuwa kuwafukuza
kwenye machimbo hayo ni kuwanyima ajira na kwamba tayari walikuwa
wametumia nguvu na fedha katika uchimbaji.
Wakazi wa mji wa Nzega
wamepokea kwa masikitiko makubwa kauli ya Serikali ya kuwaondoa
wachimbaji hao ambao walikuwa wanakuza uchumi wa mji huo na kuitaka
Serikali kusitisha zoezi hilo kwa manufaa ya wakazi wa Nzega.