Noumaaa!!! JAMAA ADAKWA AKIWANGA KANISANI,TAZAMA PICHA ZAKE HAPA


Vitenda kazi vyake vikiwa vimemwagwa chini.

Akiwa amevua shati huku akiwa anaombewa akiwa eneo la kanisa.  Jamaa  alikuwa akijihusisha na vitendo vya kishirikina, akiwa chini ya wanamaombi wa kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha mara baada ya mtu huyo kukamatwa usiku wa kuamkia leo wakati wa maombi kanisani hapo ambapo ametoa maelezo mbalimbali namna alivyokuwa akishiriki katika vitendo hivyo vya kishirikina.
Vitendea kazi vya jamaa
Katika hali isiyo ya kawaida mtu huyu ajulikanaye kwa jina la Shabani Hamis amenaswa akiwa anafanya uchawi katika kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha.

Matukio ya kunaswa wachawi yamekuwa mengi kanisani hapo kutokana na uweza wa Mungu unaojidhihirisha kupitia Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Frank Andrew.

Pamoja, na kukutwa bila nguo mtu huyo aliyekuwa amebeba vifaa ambavyo kwa mujibu wa maelezo yake, huvitumia kuwanga na kupaa ni pamoja na tunguli na kikapo cha mkoba wa uchawi. Tukio hilo la aina yake limetokea Usiku wa saa sita, wakati mkesha wa maombi ukiendelea kanisani hapo.

Baada ya maombi makali ya kuharibu uchawi katika anga la Arusha, ikafuatiwa na tukio hilo. Mungu ni mkuuu maana hapana uchawi wala Uganga juu ya watu wa Mungu.
 
Picha kwa hisani ya Ufufuo Crew.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post