Ni Balaaa,Usitake kusimuliwa!!! TAZAMA HAPA UONE JINSI SHINYANGA WALIVYOFUNIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI,KATIKA KIJIJI CHA KAGONGWA WILAYANI KAHAMA


Ni katika eneo la ofisi ya afisa mtendaji kijiji cha Kagongwa kata ya Kagongwa katika moja vituo vya kuchotea maji muda mchache tu baada ya kukata utepe kuzindua mradi wa maji katika vijiji vya Kagongwa na Iponya.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Ally Nassoro Rufunga akiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa pamoja na wakazi wa eneo hilo wakishuhudia tukio zima la uzinduzi rasmi wa mradi huo wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa

Mkuu wa mkoa akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wajumbe wa kamati ya maji katika kijiji cha Kagongwa bi Annastazia Mayai  muda mchache tu baada ya kuzindua rasmi mradi huo wa maji.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akimtwisha ndoo ya maji bi Regina Nyanda kwenye eneo la mradi wa maji katika kijiji cha Kagongwa ikiwa ni kiashirio cha kwamba sasa wananchi  11,294 wa vijiji vya Kagongwa na Iponya wanaanza kunufaika na mradi huo na kuwapunguzia adha ya muda mrefu ya maji.

Awali kabla ya mkutano wa hadhara,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiweka jiwe la msingi katika tenki la mradi wa maji ambayo chanzo chake ni kisima kirefu katika kijiji cha Kagongwa na Iponya katika kata ya Kagongwa wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.Mradi huo wa maji umeanza kujengwa tarehe 11,Juni 2013 na utarajiwa kukamilika Machi 30 mwaka huu,ikiwa jumla ya gharama za mradi huo ni shilingi 432,884,055/= na pindi ukikamilika watu 11,294 watanufaika na mradi huo.Kulia ni
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja.


Msanii wa nyimbo za asili maarufu kwa jina la MWANAKWELA kutoka Kahama akiwa na kikundi chake wakitoa burudani katika eneo la mkutano wa hadhara ulifanyika katika ofisi ya afisa mtendaji wa kijiji cha Kagongwa na kuhudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga,wakuuwa wilaya zote za Shinyanga,wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama,wenyeviti wa halmashauri,wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa,wakurugenzi watendaji wa mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira mkoa,viongozi wa dini na siasa,wanahabari,wananchi n.k
Eneo la mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kagongwa wageni waalikwa wakifuatilia kilichokuwa kinajiri

Jukwaa kuu wakiangalia burudani iliyokuwa inaendelea katika sherehe za siku ya maji duniani.

Burudani za aina mbalimbali zinaendelea
Wanafunzi wa shule ya msingi Kishima A na B za wilayani Kahama wakiimba wimbo wa maji katika eneo la mkutano leo
Kikundi cha IPYAGULA kutoka Kahama kikitoa burudani katika siku ya maji duniani ikiwa na kauli mbiu inayosema uhakika wa maji na nishati.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akizungumza leo wakati kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa,ambapo pamoja na mambo mengine alisema ujenzi wa miradi ya maji mkoa Shinyanga ni kilelezo cha utekelezaji wa ilani chama cha mapinduzi huku akiwapongeza viongozi mkoani Shinyanga kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi mkoa kwa kufanikisha miradi ya maji,kati ya miradi hiyo vyake ni maji kutoka ziwa victoria,visima virefu na vifupi na visima vya asili.Mgeja pia alimwaga sifa kwa serikali ya awamu ya nne chini ya rais Jakaya Kikwete kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile maji,barabara,hospitali,zahanati n.k.
Injinia wa maji mkoa wa Shinyanga bi Elizabeth Kingu akiwasalimia wakazi wa wilaya ya Kahama wakati kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa,ambapo mambo kadha wa kadha yamesisitizwa na viongozi ni wananchi kutunza miundo mbinu ikiwa ni pamoja kupanda miti katika maeneo ya miradi ili kutunza uoto wa asili lakini pia kulipia ankara zao za maji kwa wakati na kuwa tayari kuchagia miradi hiyo ya maendeleo ili iwe endelevu
Wanachi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ambaye pamoja mambo mengine alisema maudhui ya ya kauli mbiu ya wiki ya maji mwaka huu ya UHAKIKA WA MAJI NA NISHATI yanatokana na ukweli kwamba maji na nishati vinategemeana kwani inaonesha kuwa asilimia kubwa ya nishati huzalishwa kwa nguvu ya maji na pia karibu asilimia 8 ya nishati duniani hutumika kuendesha mitambo ya kuazlisha maji,kutibu maji na kusukumia maji hadi yanapohitajika

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Ally Nassoro Rufunga akitoa hotuba yake leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa yaliyofanyika wilayani Kahama,ambapo alisema maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kwa kiasi kikubwa kuwahamasisha wananchi kuhusu utekelezaji wa sheria,sera na programu za maji zinazoendelea hapa nchini.Alisema katika utekelezaji wa sera ya maji ya mwaka 2002 umelenga kuboresha usambazaji wa huduma za maji ,utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji na uchangiaji wa gharama za miradi ya maji pamoja na gharama za uendeshaji na matengenezo.


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga alitumia fursa hiyo kuipongeza halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kwa kutekeleza vizuri miradi ya maji kimkoa na nchi nzima kupitia mpango wa BRN ambapo wananchi wanatakiwa kuchangia asilimia 2.5 ya gharama za miradi ya maendeleo hususani fedha za kuanzia shughuli za uendeshaji pindi miradi inapokamilika.Amesema  Kishapu imefanya vizuri kwa  kuchangia shilingi 56,840,000/= kati ya sh.97,503,149/= sawa na 58%, na halmashauri mwisho katika ya 6 za mkoani Shinyanga  ni ile ya manispaa ya Shinyanga ambayo imechangia shilingi 3,534,000/= kati ya sh.55,677,900/= sawa na 6.3%.
Mkuu huyo wa mkoa alisema katika kuboresha huduma ya maji mijini,mkoa wa  Shinyanga unaendelea kushirikiana na mamlaka tano za maji safi na usafi wa mazingira ambazo ni KASHWASA,SHUWASA,KUWASA,Isaka na Mhunze.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga Justine Sheka akizungumza kwa niaba ya wenyeviti wa halmashauri 6 za wilaya mkoani Shinyanga ambapo aliipongeza viongozi wa CCM kushirikiana na viongozi wa mkoa hadi ngazi za chini katika kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inatekelezwa katika jamii

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga aliyekuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji duniani akikabidhi pesa zilizotokana na mchango watu mbalimbali waliofika katika sherehe hizo kwa ajili ya kuvipa nguvu vikundi vya burudani vilivyokuwa katika sherehe hizo,jumla ya shilingi laki 1 na elfu 47 zilipatikana ,kila kikundi kikapewa kiasi chake,wengine elfu 30,wengine elfu 25.Pichani ni MWANAKWELA akipokea pesa kutoka kwa mkuu wa mkoa,Lakini hapo anashikana mkono na mwenyekiti  wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja baada ya kuchukua pesa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post