Maajabu!!! KUTANA NA MWANABAIOLOJIA WA KIKE ANAYEHUDUMIA TEMBO YATIMA NCHINI ZAMBIA

Mwanabiolojia ambaye ameondoka nchini kwake UK baada ya kuhitimu masomo yake ya Chuo Kikuu, Rachael ameyaelekeza maisha yake katika kuwasaidia watoto wa tembo ambao wameachwa bila mama zao kutokana na ujangiri ambao wamekuwa tishio kwa wanyama hao sehemu mbalimbali Duniani.

Rachael anaifanya shughuli hiyo katika hifadhi ya taifa ya wanyama pori ya Kafue ambayo ni kongwe na yenye eneo kubwa zaidi nchini Zambia.
Siyo tu huwa anafanya kazi ya kuwatibu na kuwapa mahitaji muhimu wanyama hao, bali pia kutumia saa 24 akifanya shughuli za hatari kuwaokoa tembo ambao wapo katika hatari ya maisha yao.
Rachael ameingia nchini Zambia mwaka 2008 baada ya kufanya kazi za wanyama akizunguka maeneo kadhaa Duniani. Rachael, amepata elimu yake Royal Holloway College, jirani wa Egham, Surrey.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post