KUHUSU AJALI YA BASI LA SAIBABA,DEREVA APOTEZA MAISHA PAPO HAPO MAJERUHI 22

Mtu mmoja amekufa papo hapo na wengine 22 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya saibaba walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es salaam kwenda Kyela mkoani Mbeya kupinduka katika kijiji cha Mwambegele wilayani Rungwe.
 
Safari ya basi la kampuni ya Saibaba lenye namba za usajili T 973 AVW kutoka jijini Dar es Salaam kwenda wilayani Kyela imeishia kwenye kona kali ya Mwambegele wilayani Rungwe, baada ya basi hilo kupinduka, ambapo mkuu wa wilaya Rungwe Crispine Meela ni miongoni mwa watu ambao wamewahi kufika kwenye eneo la tukio na hapa anaelezea chanzo cha ajali hiyo. 
 
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Rungwe waliokolazwa majeruhi,Mandana Stanford Mwakatage amethibitisha kupokea mwili wa mtu mmoja na majeruhi 22 wa ajali hiyo huku akisema kuwa baadhi ya majeruhi hali zao bado sio za kuridhisha.
 
Imeelezwa kuwa mwendo kasi wa basi hilo ndio  umewasababishia ajali ambayo imesababisha kifo cha dereva wa basi hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post