JAMAA ACHEZEA KICHAPO BAADA YA KUGONGANISHA MADEMU,TAZAMA PICHA HAPA

Eric 
Mkiambiwa michepuko sio dili nyie mnakomaa mnajiona vidume kuwa na warembo wengi.. katika hali ambayo iliwashangaa watu wengi na kuwaacha midomo wazi wakazi wa mji wa kigamboni jijini Dar es salaam ni pale jamaa mmoja sharobaro mzuri tu alipochezea kichapo baada ya kugonganisha magari (wanawake). Inasemekana jamaa huyo anasoma chuo kimoja hapa town na amekuwa na tabia ya kuwadump watoto wa kike.. 

Walioshuhudia  tukio hilo wanasema jamaa huyo aliingia katika nyumba yake aliyopanga na wakati anaingia aliongozana na msichana mwembamba hivi.. na baada ya masaa kama mawili alikuja dada ambaye alipakizwa kwenye bodaboda na ndipo alipogonga na kufunguliwa mlango.. 

Baada ya hapo watu walisikia malumbano huko ndani mara pakawa kimya na ndipo jamaa alipotoka akiwakimbiza mabinti hao huku akivuja damu mdomoni na puani  jambo lililoashiria kuwa jamaa alipewa kichapo toka kwa wadada hao,,,  

Hii nadhani ni fundisho kwa wengi wetu, achana na michepuko la sivyo kama sio kukwaa ngoma huko bila shaka utaambulia kichapo kama huyu jamaa
credit- usacanadatanzania

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post