Hii kali!! HOI KWA KUNYWA DAWA YA KIENYEJI ALIYOPEWA NA MGANGA WA KIENYEJI ILI KUBAINI WEZI WA NG'OMBE WAKE

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Pendo Kona, amepoteza fahamu na kulazwa katika hospitali ya DDH-Bunda, akidaiwa kunyweshwa dawa inayosadikika kuwa sumu na waganga wakienyeji ili kuwabaini wezi wang'ombe wake.

 Mwanamke huyo mkazi wa Bunda, anadaiwa kunyweshwa dawa hiyo ili awabaini wezi wa ng’ombe wake.
 
Pendo inasemekana aliibiwa ng’ombe wawili Januari mwaka huu, na aliamua kwenda kwa waganga wa kienyeji ili asaidiwe kuwapata wezi wake.  
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Fredinand Mtui, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 3:00 asubuhi, katika kijiji cha Mugeta, wilayani Bunda mkoani Mara.
 
  Kamanda Mtui, alisema watu hao waliojiita waganga wa kienyenyeji, waliwanywesha wanafamilia hao watatu, ili wawabaini wezi wa ng’ombe wawili, mali ya Pendo walioibiwa mwishoni mwa Januari, mwaka huu. 
 
 Kamanda Mtui, alisema mwanamke huyo alipokunywa dawa hiyo, aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu ambapo alipelekwa  katika hospitali ya DDH-Bunda kwa matibabu.
 
  Hata hivyo, alisema Polisi wanamshikilia kijana mmoja ambaye ni mtoto wa mke mwenzake na Pendo, kwani ndiye anayetuhumiwa kuwaleta waganga hao waliotoroka baada ya tukio.
Chanzo;Uhuru online

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post