Geita bwana!!!!! BAADA YA MFUNGWA KUBAKA MWANAFUNZI ,WAFUNGWA WENGINE WATOROKA GEREZANI NA KUPOTELEA MSITUNI

Ikiwa ni siku chache baada ya mfungwa wa gereza la Butundwe wilayani Geita Goefry(19) Emmanuel mwenye namba 224/20013 kutuhumiwa kubaka mwanafunzi wa darasa la tano mwenye umri wa miaka 15 katika shule ya msingi Luhuha akiwa na wenzake wakichanja kuni porini ,uchunguzi umebaini kuwepo na wafungwa wengine walishatoroka gerezani na kutokomea kwenye hifadhi ya msitu wa ButundweKwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na mkuu wa magereza mkoa wa Mwanza anayekaimu pia mkoa  wa Geita,ni kwamba wafungwa hao walitoroka Machi 6,mwaka huu saa 6 mchana wakiwa kazini chini ya ulinzi wa askari magereza wawili..

Kaimu mkuu wa magereza mkoani Geita,Raphael Mollel alipotafutwa kwa njia ya simu alithibitisha kutoroka kwa wafungwa hao.alisema kuwa,

''Wafungwa walikurupuka na kutokomea kusikojulikana kwenye Msitu ulioko karibu na shamba la gereza,zoezi la kuwafuatilia bado linaendelea'' alisema Mollel kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi(sms) baada ya kupigiwa simu na kudai yuko kwenye kikao.
Hata hivyo alipoulizwa wafungwa hao walitoroka vipi wakiwa chini ya ulinzi wa askari,alisema hana taarifa kamili na kudai kuwa atakuwa na taarifa sahihi akifika eneo la tukio.

Wafungwa hao ni Edson Fitina(24)mkazi wa Chato,Emmanuel Ernest(18)mkazi wa Buseresere wilayani Chato,Safari Moshi(20)mkazi wa Katoro wilayani Geita,na Musa Deusi(22)mkazi wa Nyarugusu wilayani Geita.

Wafungwa hao kwa pamoja walikuwa wakitumikia kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuvunja nyumba na kuiba.
Inadaiwa kuwa wafungwa hao walitoroka gerezani wakati wakiwa kazini shambani wakiwa chini ya Ulinzi wa askari wawili sajenti Gaspal na Sanjet Emmanuel na kwamba hadi kufikia jana(leo jumapili) hakuna hata mfungwa mmoja aliyekamatwa

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kamanda wa polisi mkoani Geita,Leonard Paulo alisema tukio la hivi karibuni la mfungwa anaedaiwa kubaka lilitokea saa 9 alasiri Februari 26,mwaka huu wakati mwanafunzi huyo akiwa na wenzake wakitoka kuchanja kuni.
Mfungwa huyo alipowaona wanafunzi hao alijipaka majivu mwili wote,na wanafunzi hao walipoona hivyo walikimbia na kutawanyika kila mmoja njia yake na ndipo mmoja wao alianguka chini baada ya kujikwaa kwenye mti na kisha kumbaka kwa nguvu.
Kwa mujibu kamanda Paulo Mwanafunzi huyo aliumizwa sehemu za siri,pamoja jicho la kushoto baada ya kupigwa ngumi na mfungo huyo kwa lengo la kumtaka kutii azima yake ya kumbaka.

Hadi leo hii mfungwa huyo amepandishwa mahakamani na kusomewa mashitaka wawili ambapo shitaka la kwanza ni kubaka na shitaka la pili ni kumjeruhi huyo binti na amekana mashitaka akarudishwa rumande hadi tar 20 march,chini ya hakimu Desdery Kamgisha hakimu mkazi wilaya Geita. 
Na Valence Robert-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post