CCM YAPATA PIGO KIFO CHA KADA WAKE MAARUFU MKOANI SHINYANGA

Chama Cha Mapinduzi  mkoani Shinyanga kimepata pigo Kufuatia kifo cha mmoja wa makada wake maarufu ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa CCM katika kata ya Iselamagazi wilayani Shinyanga, Paul Zephania (61) aliyefariki dunia juzi baada ya kuugua malaria tarehe 14 mwezi huu na kufariki tarehe 18 mwezi huu saa 12 jioni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, Khamis Mgeja amesema CCM itamkumbuka Zephania kwa  juhudi zake za uimarishaji wa chama alizokuwa akizifanya wakati wa uhai wake na kwamba
 ameacha pengo kubwa mbalo litachukua muda kuzibika kutokana na shughuli alizokuwa akizifanya ndani ya chama.

Akiongoza mazishi ya kada huyo kijijini kwake Iselamagazi jana, Mgeja alisema  marehemu Zephania alijiunga na chama cha mapinduzi tangu mwaka 1978 na mwaka 2002 alikuwa katibu  wa tawi  CCM wilayani humo, na mnamo mwaka 2012 alikuwa mwenyekiti wa kata ya Iselamagazi hadi mauti kumfika.

 Alisema CCM imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na kiongozi wetu shupavu ambaye amekitumikia Chama kwa mda mrefu sana (36),tangu ajiunge na CCM alikuwa mchapa kazi na haja wahi kulalamikiwa na mtu yeyote na ndio maana mnaona maelfu ya watu Mmekuja kumpumzisha kwenye makazi yake ya milele kwa sababu alikuwa mtu wa watu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post