Bad News!! KIJANA ARIPUKIWA NA SIMU NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO,ALIKUWA ANAONGEA NA SIMU HUKU AKICHAJI SIMU HIYO HUKO ZANZIBAR

 
  Habari kutoka Zanzibar zinasema kuwa kuna kijana mmoja anajulikana kwa jina la Ally Bakari Ally (20) mkazi wa Kisima Mjongoni mjini Unguja  amefariki ghafla leo jioni baada ya simu aliyokuwa anatumia kupata hililafu na kuripuka wakati akiitumia kuongea na mtu.
Habari  zilizopatikana sababu ya kifo chake ni kuwa :-
Alikuwa akichaji simu yake kwa kutumia Laptop na wakati huo huo alikuwa anazungumza na mtu kupitia simu hiyo.
Imeelezwa kuwa baada ya simu kupata joto kali(over heat),simu hiyo ilimripukia na kumuathiri sehemu za mikono,uso hasa upande aloweka simu hiyo na kupelekea kufariki dunia papo hapo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mkadam Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hili na kuongeza kuwa kijana Ally alikufa baada ya kupata mshtuko wa umeme unaotokana na simu yake iliyokuwa imewekwa kwenye chaja huku akiendelea kufanya mawasiliano
Tafadhali sambaza ujumbe huu kwa wote ili sisi tulio na tabia kama hiyo tuiache mara moja.
Pumzika kwa amani kijana Ally.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post