Arusha kama Uganda!!! UKIVAA NUSU UCHI NA MILEGEZO UNAKULA BAKORA ZA KUTOSHA HADHARANI

MAKAHABA

Uongozi na wananchi wa Kijiji cha Olgilai, wilayani Arumeru jijini Arusha umekubaliana kuwachapa viboko hadharani wanawake watakaovaa mavazi ya nusu uchi hasa vimini na vijana wa kiume wanaovaa suruali chini ya makalio ‘kata kei’.

Pamoja na hilo la mavazi, adhabu ya aina hiyo itawakumba pia wanafunzi watakaopata mimba au kuozeshwa na kuacha masomo wakiwa na umri mdogo, lengo likiwa ni kukomesha tabia hizo kwa vile zimekithiri kijijini hapo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Olgilai, Godson Boazi katika barua yake ya Januari 24, mwaka huu kwa viongozi wa makanisa kijijini hapo, aliwaomba kuunga mkono hatua hiyo katika kurekebisha tabia ndani ya jamii yao.
mlegezo

“Viongozi wa dini tunafahamu kazi kubwa ya kutunza kundi la Mungu likae kwenye maadili mema. Hivyo basi tunaomba mtusaidie jukumu hili ambalo tumeambatanisha kwenu kwa barua,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.
Barua hiyo inaendelea kueleza:

“Vijana wa kiume wanaovaa mlegezo, uendeshaji ovyo wa pikipiki, wavuta bangi, watumiaji wa madawa ya kulevya, wanywa gongo na viroba, uchezaji kamari na karata. Wanaotukana ovyo barabarani na kupiga kelele za uvunjaji wa amani, wezi wa vitu vikubwa na vidogo kama kuku, ndizi, viazi, mahindi na mboga mashambani watashughulikiwa.”
Wanakijiji wote wamefurahishwa na kitendo hicho na kwa kauli moja wamepitisha azimio hilo ili kujenga kijiji chenye nidhamu na amani tofauti na hali ilivyo hivi sasa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post