Ajali!! BASI LATUMBUKIA MTONI NA KUJERUHI ABIRIA HUKO MAKETE

Habari zilizotufikia ni kwamba basi la kampuni ya Japanese Express linalofanya safari zake kati ya Makete - Njombe, limetumbukia kwenye mto eneo la Lwamadovela wilayani Makete

Basi hilo lilikuwa likitokea Njombe kwenda Makete na ajali hiyo imetokea jana  majira ya saa 11 jioni kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo

Wapo baadhi ya abiria waliojeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Ikonda Consolata

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post