AFARIKI BAADA YA KULIPUKIWA NA MAFUTA YA PETROLI

Watu watatu wamekufa wilayani Tarime katika mazingira tofauti akiwemo anayeuza mafuta ya petroli kwa vidumu aitwaye Itembe Gabriel Itembe (36) ambaye alilipukiwa na mafuta wakati akimpimia mafuta mteja wake huku akiwasha kibatari.

Kamanda wa Polisi Tarime Rorya Kamishina msaidizi, Justus Kamugisha alisema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 22 usiku katika Kijiji cha Borega tarafa ya Inchage.

Kamanda Kamugisha alisema kwamba Machi 24 mkazi wa Kijiji cha Ziba Wilaya ya Igunga  Tabora aliyefahamika kwa jina Masele Mathias ( 28) alidondoka na kufa kutoka kwenye lori lenye namba za Usajili T 531 ASB likivuta tela  namba T 128 AWP.

Ajali hiyo ilitokea kijiji cha Makongoro kata ya Rabuor katika barabara kuu itokayo Mwanza kwenda Sirari na Kenya.

Katika tukio jingine, mwili wa mwanaume anayekadiriwa kuwa na umrikati ya miaka 38 na 40 uliokotwa vichakani katika kijiji cha Kangariani kata ya Itiryo tarafa ya Ingwe.
via>>eddy blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post