Usisimuliweee!!!JIONEE MWENYEWE TUKIO ZIMA LA UZINDUZI WA KITUO CHA ELIMU YA AWALI CHA NDALA MJINI SHINYANGA,MEYA AONGOZA ZOEZI ZIMA

Ni katika  Kituo cha Makuzi na Malezi ya awali ya mtoto cha Ndala katika Manispaa ya Shinyanga ambako leo jioni kumefanyika uzinduzi rasmi wa kituo hicho ,ambacho kimejengwa kwa ushirikiano baina ya wananchi wa Ndala,Shirika la Save the Children International na Raleigh International kupitia ufadhili wa Lara Foundation.Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam(wa pili kutoka kushoto).Wa kwanza kulia ni mkurugenzi wa shirika la Raleigh International Tanzania bwana Alex Page
Wafanyakazi wa kujitolea(Volunteers) kutoka shirika la Raleigh International (raia wa nchi za ulaya)ambao wamekuwepo katika kata ya Ndala kwa takribani miezi minne sasa na hivi karibuni watarudi kwao baada ya kutoa elimu kwa wakazi wa Ndala kuhusu umhimu wa kujitolea katika shughuli za maendeleo katika jamii.Hapa wakiwa katika eneo la kituo  hicho cha elimu ya awali Ndala wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo hicho ambacho kitalea watoto wenye umri kuanzia miaka mitatu hadi 6
Kulia ni Meneja wa Shirika la Save the Children bwana Augustino Mwashiga akisoma risala kuhusu ujenzi wa kituo hicho(AKITUMIA LUGHA YA KISWAHILI) na wa kwanza kushoto ni Mratibu wa ulinzi wa mtoto kutoka shirika la Save the Children akisoma risala hiyo kwa Lugha ya Kiingerza huku afisa mtendaji wa kata ya Ndala bwan  Dickson Venance akisadia katika kuwapatia kipaza sauti.Miongoni mwa mambo yaliyogusiwa katika risala ni kuhusu umuhimu wa kumalizika kwa ujenzi wa kituo hicho ulioanza mwaka 2013,ambapo kituo hicho ni muhimu sana kwa mstakabali na maendeleo ya mtoto wa Ndala kutokana na kituo hicho kuwa fursa muhimu kwa watoto wenye umri wa miaka 3 hadi 6 kujifunza kusoma,kuandika na kuhesabu lakini pia kituo hicho kuchangia kuongeza uelewa wa watoto hasa kwa lugha ya Kiwahili ambayo ni lugha ya kufundishia
Mwenye suti kulia ni mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika kituo cha Kituo cha Makuzi na Malezi ya awali ya mtoto cha Ndala katika Manispaa ya Shinyanga,ambapo alilishukuru shirika la Raleigh International kushirikiana na Shirika la Save the Children lakini pia wafadhili wa wa ujenzi wa kituo hiocho Lara Foundation na kusifu hatua hiyo huku akiwataka wananchi wa kata ya Ndala kutunza kituo hicho pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kupeleka watoto wao katika kituo hicho kwni kitasaidi watoto wanaojiunga kukuza uelewa wao,kundeleza vipaji vyao na kuongeza uwezo wa kufikiri na kutambua mambo.Lakini pia akaongeza kuwa  manispaa ya Shinyanga itaangalia namna ya kusaidia kituo hicho cha elimu
Wakazi wa kata ya Ndala wakiwemo watoto wakiwa katika eneo la kituo hicho cha elimu ya awali wakifuatilia kilichowa kinajiri,ambapo kitasaidia kwa kiasi kikubwa katika mchakato mzima wa mtoto kujifunza na kwamba inategemewa watoto takribani  50 watakaojiunga na kituo hicho wanatarajiwa kuwa waelewa na wepesi wa kujifunza na kufundishika hasa watakapojiunga na darasa la kwanza
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akikata utepe katika moja ya majengo wakati wa ufunguzi rasmi wa kituo hicho,ambapo majengo mawili yenye chumba kimoja cha darasa,ofisi ya walimu,jiko ,vyoo na uzio hadi kukamilisha ujenzi wake takribani milioni 48 zimetumika.
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akikata utepe katika moja ya majengo wakati wa ufunguzi rasmi wa kituo hicho,ambapo majengo mawili yenye chumba kimoja cha darasa,ofisi ya walimu,jiko ,vyoo na uzio hadi kukamilisha ujenzi wake takribani milioni 48 zimetumika.

Wafanyakazi wa kujitolewa kutoka nchi ya Uingereza na mataifa mengine na wakazi wa Kata ya Ndala wakishuhudia zote la kukata utepe katika majengo mawili ya kituo hicho cha elimu ya awali lililokuwa linafanywa na Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam

Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akishikana mikono na baadhi ya watoto ndani ya darasa lao ambao tayari wamejiunga na kituo hicho cha elimu awali Ndala,ambapo katika kituo hicho watoto hap watapata angalau mlo mmoja wakiwa kituoni hapo hivyo kutumikam kufikisha ujumbe kwa wazazi kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa watoto
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akishikana mkono na mmoja wa wafanyakazi wa kujitolea kutoka shirika la Raleigh International ambao wameweza kukaa katika kata ya Nadala  kwa miezi minne kwa usimamizi wa kamati ya kituo,mtendaji wa kata ya Ndala,mwenyekiti wa Mtaa na kamati ya maendeleo ya kata kwa kukaa vizuri na wageni hao
Picha ya pamoja mgeni rasmi na wafanyakazi wa kujitolea kutoka Raleigh International baada ya uzinduzi.Mnamo mwaka 2011 shirika la Save the Children kwa kushirikiana na jamii,wazazi na serikali za kata na vijiji lilisaidia kuainzisha vituo vya malezi na makuzi ya awali.Mwaka huo likafanikiwa kuanzisha vituo 11 ambapo 7 vipo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na vingine 4 viko katika manispaa ya Shinyanga,kati ya vituo hivyo 11,kituo cha Ndala kilikuwa hakina eneo maalum la watoto kusoma na kuwasabaisha kuhama hama na leo ndiyo furaha yao kwani hapo ndiyo patakuwa makao yao kwa ajili ya kujifunzia


Picha ya pamoja,mgeni rasmi,wafanyakazi wa Raleigh International na watoto ambao wamejiunga na Kituo cha Makuzi na Malezi ya awali ya mtoto cha Ndala katika Manispaa ya Shinyanga
Wafanyakazi wa Raleigh International wakiendelea kupiga picha na watoto mara baada ya mgeni rasmi kufanya uzinduzi wa kituo hicho rasmi.
Burudani za aina mbalimbali nazo zilikuwepo kusindikiza zoezi la uzinduzi,ngoma inaendelea kama unavyoona hapo juu. Ujenzi wa kituo cha Ndala ulianza rasmi mwezi Oktoba mwaka 2013 kwa Save the Children kushirikiana na shirika la Raleigh International,watumishi wa kujitolea,jamii,walimu wa kituo,kamati ya kituo na mafundi kutoka jamii ya Ndala.Pesa za ujenzi huo zimetolewa na Lara Foundation

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments