Updates!!! WANAFUNZI WALIOPEWA MAJINA FEKI GEITA SASA KUANDAMANA HADI KWA MKUU WA MKOA,AFISA ELIMU AJICHANGANYA


Sakata la wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyugwa katika kata Nyugwa wilayani Nyangh’wale mkoani Geita kuhusu kupewa majina ya bandia limechukua sura mpya baada ya wanafunzi hao kukubalina kufanya maandamano makubwa kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Geita Saidi Magalula endapo  serikali haitawachukulia hatua mwalimu mkuu wa shule hiyo pamoja na afisa elimu wa sekondari kwa kuuza majina ya wenzao 11 na kuwapa majina bandia.

Hatua hiyo ya kufanya maandamano imeafikiwa leo baada ya afisa elimu wa sekondari wa wilaya Bi, Mosha kufanya kikao katika ukumbi wa shule hiyo na kuwaambia wanafunzi wote 11 walifutiwa matokeo yao kwa kukosa majina yao hawatakiwi  kuonekana shuleni kwani wakiendelea kukaa hawatafanya mtihani wa kidato cha nne na wazazi wao wanatakiwa watafute utaratibu mwingine.

Kitendo cha afisa elimu huyo kufanya kikao
na kuwaambia  wanafunzi 11 hawatakiwi kuonekana katika maeneo ya shule kimezua taaruki kubwa kwa wanafunzi pamoja  na wazazi waliokuwemo kwenye kikao hicho  huku ikidaiwa kuwa yeye mwenyewe ndiye aliyewaamuru wafanye mtihani kwa kutumia majina yasiyo yao katika mtihani wa kuingia kidato cha tatu mwaka jana na kuahidi kuwasaidia  na  mpaka sasa hajachukua hatua hivyo  kuonekana yeye anahusika na mkuu wa shule hiyo kuuza majina ya watoto wao na kuwapa ya bandia tena kwa pesa kuanzia shilingi(25000) hadi (30000) na kudai majina yao ya awali yako mkoani yanatakiwa yatafutwe.

Mmoja wa wanafunzi aliyebadilishiwa jina lake la awali alikuwa anaitwa Jen Pendo na kubatizwa la badia la Jasinta Zakaria alikuwa na haya ya kusema..........

 “Nashangaa kuona afisa elimu anatugeuka na huku yeye ndiye aliyetusaidia  kufanye  mtihani na aliahidi kuwa  atalishugulikia na an hawatutakiwi kuonekana katika shule hii bali wazazi wafanye utaratibu mwingine.’’

“Kwa kweli namshaanga huyu afisa elimu kwani mimi mwenyewe nilikataa baada ya kuona jina si langu lakini akaniomba nilifanyie jina hilo na atalishugulikia nashangaa hata mimi ananigeuka ,sasa niende wapi na nimepoteza muda mwingi na kulipa michango yote na je pesa yangu watarudisha? naiomba serikali ituasaidie kutatua mgogoro huu ‘’alieleza Jen Pendo

Wakati huohuo wazazi  waliokuwepo kwenye kikao hicho  cha wanafunzi na walimu wa shule hiyo wamlalamikia kitendo hicho na kukiita cha kinyama na cha kikatili huku nao wakiomba serikali kuingilia mgogoro huo na kuwachukulia hatua kali na ikiwezekana wapewe adhabu kali ama wafukuzwe.

 “Mimi kama mzazi naona mwalimu hawezi kuuza majina peke yake ,maafisa elimu wote naona watakuwa wanajua wote wachukuliwe hatua lakini pia nashanga kuona mwalimu mkuu bado yupo hapa na wakati amefanya hujuma zote hizi”,alisema mzazi aitwaye Pendo kisabo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post