MWANAMKE ACHINJWA KAMA KUKU BAADA YA KUGOMA KUFANYA TENDO LA NDOA NA MME WAKE

NewsImages/2213346.jpg

Mkazi wa mmoja mkazi wa kijiji cha Tazengwa wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Juma Kiyabo (45) amemchinja mke wake, Wande Monera (34), kabla ya mwenyewe kunusurika kifo baada ya kujijeruhi vibaya shingoni katika jaribio la kutaka kujiua.

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Tazengwa saa 7 usiku wa Februari 16 mwaka huu, huku ikielezwa kuwa sababu ya tukio hilo ni kunyimana unyumba mara kwa mara.

Kaimu Kamanda wa Polisi, ambaye pia ni Mratibu Msaidizi mkoani Tabora, John Kauga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


Kaunga alisema taarifa za awali zinaonyesha kuwa, mtuhumiwa alikuwa akigombana na mkewe mara kwa mara kwa sababu ya kunyimwa unyumba kabla ya kuamua kuchukua hatua hiyo mbaya.


Kamanda Kaunga alisema kuwa, mtuhumiwa baada ya kufanya unyama huo, naye alijikata koo kwa lengo la kujiua, lakini hata hivyo jaribio lake lilishindikana na sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi.
Credit-Kandili yetu blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post