MAHABUSU AJINYONGA CHOONI KWA KUTUMIA TAMBARA LA KUPIGIA DEKI


MAHABUSU, Vumi Elias (30), amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia tambara la kupigia deki ndani ya choo cha mahabusu ya Kituo cha Polisi Tunduma.
 
Elias, mkazi wa Maporomoko-Tunduma, aliyetuhumiwa kwa unyang’anyi wa kutumia nguvu katika eneo la Tunduma wilayani Momba, alifariki dunia jana, saa 12 asubuhi muda mfupi baada ya kufikishwa katika Kituo cha Afya Tunduma kwa matibabu.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Robert Mayala, alisema Elias aliingia choo cha mahabusu saa 10 alfajiri na kufanya jaribio la kujinyonga kwa kutumia nguo ya kupigia deki.
 
CREDIT: EDDY BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post