Ukatili huu mpaka lini? WANAWAKE WAWILI WAUAWA MBEYA,MMOJA AKATWA KOO,MWINGINE KWA KUPIGWA MANGUMI NA MATEKE


Wanawake wawili wameuawa na waume zao katika matukio mawili yaliyohusisha mmoja kukatwa koo na mumewe.
 
Wanandoa hao waliuawa wilayani Chunya mkoani Mbeya, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi  mkoani Mbeya Ahmed Msangi.
 
Kamanda alieleza kuwa Agnes Daudi, anadaiwa kuuawa na mumewe  Thomas Msukuma na kwamba mwili wake ulikutwa ukiwa umekatwa koo na kutelekezwa kwenye kibanda walichokuwa wakiishi pamoja enzi za uhai wake.
 
 Alisema tukio hilo lilitokea saa 1:00 asubuhi katika kijiji cha Shoga wilayani Chunya.
 
Katika tukio la pili lilitokea  saa 12:00 jioni kijiji cha Landan Dafroza Gidion (18) aliuawa kwa kupigwa ngumi na mateke mashambulio yaliyodaiwa kufanywa na mumewe Juma Januari.

Alisema sababu za mauaji hayo ni  chuki za mapenzi.
CHANZO: NIPASHE

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post