CCM WAPATA KATA ZOTE 3 UCHAGUZI WA MADIWANI HUKO IRINGA

 
Wafuasi wa CCM kata ya Nduli  wakiwa  wamemnyanyua  juu  juu  aliyekuwa mgombea  udiwani kata ya Nduli Bw Mtove  baada ya  matokeo kumpa ushindi wa kishindo leo 

CHAMA  cha  mapinduzi (CCM)  mkoa  wa  Iringa  kimefanikiwa  kutetea kata  zake  zote tatu ambazo  leo   wananchi  wameshiriki  kupiga kura  kuwachagua madiwani  kufuatia nafasi hiyo kuwa wazi baada ya madiwani wake kufariki  dunia  huku chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kikishindwa  vibaya katika  uchaguzi huo.

Mbunge  wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ambae  alikuwepo  eneo la Nduli  akifuatilia  matokeo  ya uchaguzi huo pamoja na  wafuasi wa Chadema  alilazimika  kuondoka katika eneo hilo  baada ya  kubaini kuwa hali ya ushindi kwa Chadema ni ndoto.
 
Huku   wafuasia  wa  CCM  wakionekana  kumpongeza  aliyekuwa mgombea wa CCM kata ya Nduli pamoja na  kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa  Hassan Mtenga kuwa  kazi  yake imeonyesha inaonyesha  wazi  safari yake ya  kulitwaa jimbo la Iringa mjini .

Katika  Matokeo hayo ambayo hadi sasa  majira ya saa 12.50  bado msimamizi wa uchaguzi kutangaza CCM inaongoza kwa kura 810 huku  Chadema  wakifuatia kwa kura 491 
Mbali ya  matokeo  hayo ya kata ya  Nduli pia  CCM imeshinda kata ya Ibumi na Ukumbi zote za  wilaya ya  Kilolo.
 

Na Francis Godwin

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post