Sakata la wanaCCM kucharangwa Mapanga Kahama!!!! MBUNGE KASULUMBAYI WA CHADEMA APATA DHAMANA,WENGINE 12 WAKOSA DHAMANA

Mbunge wa  Maswa Mashariki Sylivester Kasulumbayi (CHADEMA)-Picha kutoka Maktaba ya Malunde1 Blog
Mbunge wa  Maswa Mashariki Sylivester Kasulumbayi (CHADEMA)  aliyekuwa anashikiliwa kwa kosa la kujeruhi wanachama sita wa CCM  ameachiwa kwa dhamana huku wenzake 12  wa chama hicho wakirudishwa rumande kwa kushindwa kukidhi masharti ya dhamana.

Akisoma uamuzi wa kuwaachia watuhumiwa hao wanaokabiliwa na kesi ya kuwashambulia kwa mapanga wafuasi sita wa CCM hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya ya kahama Gadiel Mariki amesema kwa makosa kama hayo dhamana yake huwa iko wazi.

Mariki amesema kuzuia dhamana inategemea na mwenendo wa
mashtaka ambapo katika cheti cha kiapo cha kuzuia dhamana hiyo kilichotolewa na polisi masuala ya msingi hayakuzingatiwa na kufanya hati kuwa batili.

Amesema kufuatia mapungufu hayo ikiwa ni pamoja na maelezo ya wagonjwa watatu kuwa mahututi haijaonesha mtoaji wa taarifa hiyo ninani hivyo hati hiyo ni batili.

Pamoja na kubatilisha hati hiyo na kuweka dhamana wazi, wadhamini wa watuhumiwa 12 akiwamo diwani wa kata ya Buselesele wamekosa sifa na kufanya warudishwe gerezani, huku wadhamini wa mbunge kasulumbayi hati zao zikiwa sawa.


Kasulumbayi na wenzake wanashitakiwa kwa makosa sita yakiwamo matano ya kujeruhi na moja la kuharibu mali za wanachama wa CCM katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya ubagwe, na kesi hiyo itatajwa tena feburuali 20 mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post