Inasikitisha!!! MWALIMU AJINYONGA CHOONI,CHANZO CHADAIWA KUWA NI MSONGO WA MAWAZO

NB-Picha haihusiani na tukio katika habari
Mwalimu  wa shule ya msingi Mwang’osha kata ya Nyamalongo wilaya ya Shinyanga  Vijijini Christipian Mafuru (24) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani katika choo kilichopo nyumbani kwake.

Akizungumza  na waandishi wa habari Mwalimu mkuu wa shule hiyo Frida Maleko amesema  marehemu Mafuru amegundulika akiwa amejinyonga juzi majira ya saa tisa na nusu alasiri.

Amesema  baada ya mwalimu huyo kutoonekana shuleni hapo kwa muda mrefu walijaribu kumpigia simu  marehemu bila mafanikio na kuamua kuondoka na walimu wenzake kwenda nyumbani kwake na kukuta mlango umefungwa huku simu ikiita ndani bila ya kupokelewa.

Maleko amesema  walichukua  jukumu la kuvunja dirisha na mara baada ya kufanikiwa kuingia ndani   walikuta ujumbe wa maneno mezani uliokuwa umeandikwa na marehemu ukisomeka kuwa.......

"MSONGO WA MAWAZO UMENILAZIMU NIFANYE HIVI,POLENI SANA WALIMU WENZANGU,SAMAHANI WAZAZI WANGU,KWA HERI MWANANGU REY"

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Shinyanga  Evarist Mangalla amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post