Mapanga Tena Kahama!!! MAMA NA MTOTO WAVAMIWA NA KUKATWA KATWA MAPANGA

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla
Wanawake wawili wakazi wa  kijiji cha Ngokolo kata ya Bukomela wilaya ya  Kahama mkoani Shinyanga wameuawa kikatili kwa kukatwa katwa mapanga sehemu za kichwani na kisogoni na watu wasiojulikana wakati wakipika chakula cha usiku nyumbani kwao.

Tukio hilo limetokea juzi  saa moja na nusu usiku ambapo wanwake hao (mama na mwanaye) walivamiwa na watu hao kisha kufanya unyama huo na kutokomea kusikojulikana.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala  amewataja wanawake waliouawa kuwa ni Helena Charles(30) na mama yake aitwaye Mlu Nambo(50) wote wakazi wa kijiji cha Ngokolo ambao walifariki dunia papo hapo kufuatia kuvuja damu nyingi.


Aidha amesema chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa na tayari mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi na wengine waliohusika na mauaji hayo wanaendelea kusakwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post