LADY JAY DEE AJIFUNZA KARATE,SIJUI KUNA NINI!!!!!!!

Moja kati ya surprises zilizokuwepo wiki iliyopita ni pamoja na habari ya Lady Jay Dee aka Anaconda kujifua kikomando kuumudu mchezo wa Karate, habari iliyoambatana na picha zikimuonesha akifundishwa mchezo huo tena akiwa ndani ya mavazi rasmi.

Itakuwaje Jide akishakuwa fiti kwenye mitindo hatari ya karate kama Shotokan, Wado-ryu, Shito-ry na Goju-ryu? Na je, anataka kumkabili nani hasa? Haya ni kati ya maswali ambayo wengi tulijiuliza.
 
“Kwa sababu ninao muda wa ziada, halafu kukaa tu idol bila kufanya kitu saa zingine inaweza kupelekea mawazo yako kufikiria vitu vibaya. Kwa hiyo nikaona sio vibaya nikifanya mazoezi.” Alisema Lady Jay Dee aka Anaconda.
Alipoulizwa kama kuna mtu anataka kupigana naye alisema hakuna mtu ila anajiweka fiti tayari kwa lolote.
“Hapana ni kutaka kujiweka fiti unajua kufanya mazoezi sio kwa ajili ya kutaka kupigana na mtu, ni wewe mwenyewe tu uwe vizuri ili jambo likitokea ujue jinsi ya kuji-protect.” Ameeleza.
Mkali huyo wa Joto Hasira amedai kuwa ana mwalimu mzuri na kwamba yeye pia ni mwanafunzi mwenye bidii.
credit: babamzazi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post