KUTANA NA KUKU WENYE NGOZI NYEUSI TII !!!, HUATAMIA MAYAI YA NDEGE WENGINE BILA KINYONGO

Kuku weusi
Aina kadhaa za kuku weusi  hupatikana barani Asia, lakini  kuku au ndege aina ya Silkie wa huko China, ndiyo maarufu zaidi.  Ndege hao, kama majina yao yalivyo, huwa wana manyoya yanayofanana na hariri.
Hata hivyo, chini ya uzuri wote huo, ndege hao wana ngozi nyeusi tii!  Ndege hao huuzwa katika nchi za magharibi kama mapambo, ambapo nchini China ni kitoweo cha hali ya juu kwani nyama yake  hupendwa sana.  Pia ndege hao huchukuliwa kama ‘mama wema’ kwani wanaweza kuatamia mayai ya ndege wengine bila kinyongo.
Black-Chicken
Wachina huwaelezea ndege hao kama “kuku wenye mifupa myeusi” au  “wu gu ji” na wamekuwa wakiwala kwa kuamini nyama yao ina tiba tangu karne ya saba au ya nane ambapo wanawake huila kwa ajili ya kuimarisha afya zao baada ya kujifungua. 
 Pia nyama hiyo inaaminika kuimarisha mapafu, tumbo na damu ikiliwa.  Wachina huitumia nyama ya ndege hao kwa kutengeneza supu yake na kuichanganya na viungo na matunda mbalimbali kwa ajili ya tiba.

Utafiti uliofanywa na kuchapishwa mwaka 2011 ulionyesha kwamba hali hiyo ya kipekee ya ndege hao aina ya Silkie ambayo inajulikana kama ‘fibromelanosis’ inatokana na mabadiliko katika jeni.  Mabadiliko hayo kisayansi  huenda sambamba na kuongezeka kwa chembechembe za  rangi ambazo huzifanya sehemu za ndani (mwilini) na mifupa kuwa nyeusi.

Ndege hao pia wana chembechembe za aina ya ‘carnosine’ ambazo huongeza nguvu mwilini.  Watu wenye kutaka kuongeza ukubwa wa misuli huwatumia kwa wingi kwa nia hiyo na kama chakula chenye kuleta nguvu.  Pia hutumika katika kupambana na ugonjwa wa akili wa watoto (autism), kisukari na kupambana na matatizo yanayotokana na uzee.
 
Kwa jumla ndege hao hutumiwa kama tiba ya maumivu ya viungo na kuzuia ugonjwa wa akili ujulikanao kama Alzheimer.
 
Kwa mujibu wa  utafiti wa kisayansi kuhusu kuku nchini Uingereza, mayai ya kuku weusi  ni bora kwa afya hasa yakitumika katika kupika keki.  Yakilinganishwa na mayai mengine, mayai ya kuku weusi yana kiwango kidogo cha tindikali  katika mafuta yake. 
 
 Kwa waliowahi kuila nyama yake, wanasema ina ladha kama ya kuku wa kawaida, lakini baadhi hudai ni tamu zaidi.  Je, ungependa kula nyama ya Silkie ili ufahamu utamu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post