Hatariii!! MAMBA MLA WATU AWA TISHIO GEITA,AUA WATU WAWILI NA KUJERUHI MMOJA

 

Wananchi wa kijiji cha Nyansalala katika kata ya Bukondo wilaya ya Geita wameiomba serikali ya mkoa wa Geita kuwasaidia kumuua mamba anayewinda watu  na wanyama kando kando mwa ziwa Victoria.

Wakiongea kwa nyakati tofauti juzi wananchi hao wamesema  kuwa mamba huyo amewakosesha amani wananchi wa eneo hilo mpaka kufikia kuacha kufanya kazi   katika kjijij hicho hivyo kuiomba idara ya wanyamapori mkoa huo kuweza kumwinda na kumua.

 Diwani wa kata hiyo John Magulu amesema   kuwa kuna watu 2 wameuawa na mamba huyo na kuwataja waliouawa kuwa ni Luganga Lukana (30)  na mkazi wa kijijij cha Chankorongo  na  omary Amos (12) mwanafunzi wa darasa la 4 katika shule ya msingi Mapinduzi Bukondo.

Diwani huyo  amemtaja aliyejeruhiwa na mamba huyo kuwa ni kuwa ni Tizita Luhindisa   mkazi wa kijiji cha Kitigili katika kata hiyo(48) hivyo kuiomba serikali kuwasaidia kwa hali na mali wananchi wa vijiji hivyo.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza, diwani huyo amesema  pamoja na kupeleka taarifa kuhusu mamba huyo katika ofisi za wanyama pori wilaya ya Geita lakini hawajapata msaada wowote kutoka kwenye ofisi Aidha diwani huyo amewataka  wananchi hicho kushirikiana katika kuhakikisha wanamuua mamba huyo anayesumbua wananchi kila kukicha.


 Afisa wanyama pori wilaya ya Geita Bw Msese Kabulizina amekiri kuwepo kwa mamba huyo katika vijiji hivyo na kuongeza kuwa jitihada za kumuua mamba huyo zinaendelea kwa hali na mali kuweza kumpata na kuweza kumua na kuwaomba wananchi hasa wavuvi wanaovua kando kando ya ziwa kuwa makini na waangalifu wakati wa shughuli zao.

Na Valence Robert-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post