Habari Picha!!!TAMWA YAANZA SEMINA YA SIKU 3 KWA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA KUHUSU UKATILI WA KIJINSIA

Mwezeshaji wa mafunzo kuhusu ukatili wa kijinsia yanayoendeshwa na  
       Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), bwana Deodatus Balile ambaye ni mhariri mtendaji gazeti la Jamhuri akizungumza leo katika ukumbi wa Vigimark Hotel mjini Shinyanga ambapo waandishi wa habari 20 kutoka mkoa wa Shinyanga na Simiyu wanahudhuria mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo juu ya ukatili wa kijinsia wakifanya kazi ya kikundi kama walivyoelekezwa na mwezeshaji kuhusu uelewa wao kuhusu ukatili wa kijinsia katika jamii
Semina inaendelea ambapo pamoja na mambo mengine mafunzo hayo yatawawezesha waandishi hao wa habari kuandika habari zao kwa kuzingatia usawa wa kijinsia katika jamii
Washiriki wa semina hiyo ya siku tatu iliyoanza leo wakijadili mawili matatu kuhusu mambo ya ukatili wa kijinsia ambapo mafunzo hayo yanaendeshwa na Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA)
Washiriki wa semina wakifuatilia kwa makini walichokuwa wanakijadili katika kikundi chao 
Bi Veronica Natalis kutoka Radio Faraja fm stereo akiwasilisha kazi ya kikundi chao kuhusu ukatili wa kijinsia katika semina ya siku tatu iliyoanza leo kwa waandishi wa habari mjini Shinyanga
Bwana Kadama Malunde mwandishi wa habari gazeti la Zanzibarleo na mkurugenzi wa malunde1 Blog  akiwasilisha kazi ya kikundi chake katika ukumbi wa Vigimark Hotel mjini Shinyanga katika semina hiyo ya siku 3 ya TAMWA
Mwezeshaji wa mafunzo kuhusu ukatili wa kijinsia yanayoendeshwa na  
       Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), bwana Deodatus Balile ambaye ni mhariri mtendaji gazeti la Jamhuri akifunga mafunzo kwa siku ya kwanza ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka waandishi wa habari kuzingatia usawa wa kijinsia wanapoandika habari zao na kwamba vyombo vya habari vikitumika vizuri vitasaidia katika kupiga vita ukatili wa kijinsia katika jamii

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post