Huu ni ukatili uliopitiliza!!! MWANAMME ANYONGA MTOTO WA WIKI MBILI KWA KUTUMIA MIKONO YAKE MWENYEWE HUKO GEITA


Mkazi wa kijiji cha Ibamba katika kata ya Uyovu tarafa ya Siroka wilaya ya Bukombe mkoani Geita aitwaye Shija Hamis (28) amemuua mtoto wake mwenye umri wa wiki mbili kwa kumnyonga shingo kwa kutumia mikono yake mwenyewe.

Tukio hilo limetokea tarehe 4 mwezi huu ambapo chanzo chake kinadaiwa kuwa ni ugomvi wa kifamilia ambapo inasemekana Shija Hamis alikamatwa mwezi wa pili mwaka jana kwa kosa la wizi wa mifugo wilayani Biharamulo mkoani Kagera akafungwa alipotoka mahabusu alimkuta mke wake aitwaye Julian Juma (20) akiwa mjamzito.

Imeelezwa kuwa baada ya kumkuta mke wake akiwa mjamzito jamaa alianza kumtilia mashaka mke wake kwamba huenda mimba aliyokuwa nayo siyo ya kwake.

Hata hivyo baada ya mwanamke huyo kujifungua tarehe 22 Januari mwaka huu jamaa alidai kuwa mtoto aliyezaliwa siyo wa kwake.

 Inadaiwa kuwa tarehe 4 mwezi huu jioni,Bi Juliana alikuwa anapika nyumbani kwake wakati huo huo mme wake alikuwa nje huku mtoto wao ambaye hata hivyo walikuwa hawajampa jina alikuwa amelala ndani.......

Wakati anaendelea kupika muda mchache akasikia sauti ya mtoto wao akilia na ndipo Shija Hamis akaingia ndani ili kumwangalia mtoto... lakini alipofika humo ndani alimchukua mtoto huyo na kumnyonga hadi kufa.

Habari zinasema kuwa mara baada ya kufanya mauaji hayo Shija Hamis  alitoka ndani na kuchukua baiskeli kama anatoka kidogo na kutokomea kusikojulikana.....

Aidha wakati  Bi juliana akiendelea kupika baada ya muda hakuweza kumsikia tena mtoto  akilia  huku mme wake akiwa ametoweka ,ndipo akahisi kuwa huenda  kuna kitu kimetokea akaamua kwenda ndani na ndipo akamkuta mtoto wake amenyongwa na kutupwa chini kitu kilichomfanya aangue kilio hajui cha kufanya na mme wake akiwa amekimbia kusikojulikana.

Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa ni jambo la ajabu sana kwa bwana huyo kufanya kitendo cha kinyama namna hiyo na kwamba watu wanaofanya vitendo kama hilo wanatakiwa kuchukuliwa hatua kali na ikiwezekana wafungwe kifungo cha maisha.


Kamanda wa polisi mkoani Geita Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mtuhumiwa hadi sasa jeshi la polisi linaendelea kumsaka kutokanana na kitendo alichokifanya cha kinyama dhidi ya haki za binadamu.

Na Valence Robert-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post