Balaa jingine!! MWANAMME MUUZA MIFUKO AJINYONGA ENEO LA BEACH HUKO BUKOBA,TUNAOMBA RADHI KWA PICHA UTAKAZOZIONA

Askari polisi akipanda juu ya mti ili akate kamba aliyotumia marehemu kujinyonga
Askari akiendelea na shughuli  ya kushusha mwili wa marehemu 
Marehemu akiwa juu ya mti
Baadhi ya vitu alivyokuja navyo marehemu kabla ya kujinyonga vilivyokutwa katika eneo la tukio
Mwili wa marehemu ukichukuliwa kutoka eneo la tukio na kupelekwa hospitali ya mkoa wa Kagera
Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina moja Bahati amabaye hujishughilisha na uuzaji wa mifuko ya plastiki katika stendi kuu ya mabasi mjini Bukoba amekutwa amejinyonga juu ya mti katika eneo ufukwe wa Spice  Beach Motel leo majira ya saa nane mchana.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema kabla ya kifo cha marehemu walimwona jamaa huyo akiwa na mafurushi ya vitu mbalimbali na alikuwa nafua katika eneo hilo la Beach ya Spice Motel mjini Bukoba .

Aidha taarifa za awali zinasema kuwa mapema leo asubuhi mwanamme huyo maarufu kwa uuzaji wa mifuko ya plastiki alionekana katika eneo la stendi kuu ya mabasi Bukoba akiuza mifuko hiyo kwa  wasafiri waendao mikoani.


Mwili wa marehemu umepelekwa katika hospitali ya Mkoa wa Kagera kuhifadhiwa kwa ajili ya ndugu wa marehemu kuutambua mwili wa marehemu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post