FUATILIA HAPA HISTORIA FUPI YA VALENTINE DAY


Siku ya wapendanao au Valentine's day ina historia ndefu sana,pamoja na hayo yote hii hapa ni historia  fupi ya siku hiyo kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya historia ya siku hiyo.

Asili ya siku ya wapendanao "Valentine's Day" ni St Valentine, mhubiri wa kikristo aliyekuwa akiishi karibu na mji wa Roma katika karne ya tatu wakati wa utawala wa Claudis II.

Claudis alitaka awe na jeshi kubwa akategemea vijana wangejitolea na kujiunga na jeshi lake.

Lakini vijana wengi hawakupenda vita kwakuwa hawakutaka kuziacha familia zao na watoto wao.

Claudis akafikiria akaona hawa vijana kuwakomesha waingie jeshini ni kupiga marufuku watu kuoana.Kuanzia hapo akapiga marufuku watu kuoana akitegemea vijana hawatajali sasa kujiunga na jeshi kwasababu ya familia zao.

Askofu Valentine naye kwa siri akawa anawafungisha ndoa vijana hao kwa siri.

Claudius aliposikia habari hizo aliamuru Valentine akamatwe na akahukumiwa adhabu ya kifo cha kunyongwa.

Wakati akiwa jela akisubiri siku yake ya kunyongwa Valentine alikuwa akitembelewa na vijana waliokuwa wakimpelekea maua kuonyesha wako pamoja nae.

Mmoja wa vijana waliokuwa wakienda kumtembelea ni mtoto wa mkuu wa gereza ambaye aliruhusiwa kuingia mpaka kwenye selo la Valentine "kupiga naye stori".

Inasemekana kwamba Valentine aliangukia katika mapenzi na binti huyo wa mkuu wa gereza wakati anasubiria kunyongwa.

Inasemekana kwamba muda mchache kabla hajanyongwa Valentine aliomba kalamu na karatasi na kuandika meseji yake ya kuaga akiweka sahihi "From Your Valentine" ( kutoka kwa Valentine wako )

Valentine akanyongwa tarehe 14 februari mwaka 269 AD.

Baada ya kunyongwa kwa Valentine, vijana wa Roma walianza kumuiga Valentine na kuwaandikia na kuwatumia wanawake waliowapenda salamu za mapenzi.

Tangia siku hiyo tarehe hiyo ikaanza kuhusishwa urafiki, upendo na mahaba duniani huku ikihusishwa zaidi na mambo ya mapenzi.

Siku hiyo imezidi kuwa maarufu kila miaka inavyoenda huku huku makampuni yakiigeuza siku hiyo kuwa ya biashara zaidi kwa kufanya kila kitu maalumu kwa siku ya wapendanao kionekane kuwa inabidi kiwe chekundu kuanzia kadi za salamu, maua, mpaka nguo wavaazo wapendanao inabidi ziwe nyekundu.

Kuna watu wengi pia ambao hawasherehekei siku hii kwa kuhoji umuhimu wa kuonyesha kumjali umpendaye katika siku moja tu ya mwaka badala ya siku zote 365.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post