Chadema kwanuka Tena!!! YANG'OA VIONGOZI WAKE WATANO HUKO KAHAMA,WADAIWA KUWA WAFUASI WA ZITTO

Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Kanda ya Ziwa Mashariki hii leo kimewavua uanachama pamoja na nyadhifa zao viongozi wake watano wa jimbo la Kahama kwa makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukiuka taratibu za chama hicho.

Uamuzi huo umetolewa na Mratibu wa Chedema Kanda ya Ziwa Mashariki Renatus Nzemo katika kikao kilichofanyika katika ofisi ya Kanda ya Ziwa Mashariki na kupitia mazimio hayo kabla ya kutoa uamuzi.

Viongozi waliovuliwa nyadhfa zao ni Mwenyekiti wa jimbo la Kahama Israel Barikiel, Katibu wa Jimbo Vicent Kilukilwa, Katibu Mwenezi wa jimbo Bobson Wambura, Mwenyekiti Bawacha Kasigwa Adram na Mwenyekiti Bavicha Benedict Shija.

Katika Barua yake aliyoiandika kwa viongozi hao, Nzemo amesema viongozi hao wanakabiliwa na tuhuma za kikiuka tamko la kamati kuu ya chama lililowazuaia wanachama wote kushirikiana na aliyekuwa naibu katika mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe.

Tuhuma zingine ni kushiriki kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Ubagwe kupitia chama cha TADEA, huku viongozi hao wakipita na kujinadi kuwa wako tayari kumfuata Zitto popote atakapokuwa.

Aidha Nzemo amesema viongozi hao wamekuwa wakitumia nembo ya CHADEMA kunadi chama kingine cha Alliance for change and Transparency (ACT), kinyume cha maadili ya CHADEMA katika katiba yake ya mwaka 2006.

Nzemo amesema kutokana na tuhuma hizo na zile zilizotolewa na baraza la mashauriano wilaya ya Kahama, viongozi hao wanatakiwa kukabidha ofisi na vifaa vya chama kwa baraza la wazee jimbo la Kahama mara wapatapo barua hizo.
Credit-Dunia kiganjani

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post