CCM YAWAPONGEZA WAKAZI WA UBAGWE WILAYANI KAHAMA KWA KUCHAGUA DIWANI WA CCM


Kufuatia Chama Cha Mapinduzi kupata ushindi katika uchaguzi wa diwani katika Kata ya Ubagwe wilayani Kahama mkoani Shinyanga chama hicho  kimewapongeza wakazi wa kata hiyo kwa uamuzi wao wa busara wa kumchagua diwani anayetokana na chama hicho  bwana Hamis Majogor hali ambayo inaonesha bado wana imani na mapenzi makubwa kwa CCM.


Pongezi hizo zimetolewa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Ubagwe ambapo Mgeja alisema wakazi wa kata hiyo wameonesha kwa uwazi mpana kwamba bado wana imani kubwa na CCM ambapo pamoja na vurugu na vitisho vya wagombea wa vyama vya upinzani hasa CHADEMA, ambapo baadhi ya wafuasi wa CCM walicharangwa mapanga lakini bado wananchi  wamemchagua diwani wa CCM.


Mgeja amesema CCM hivi sasa ndiyo iliyosalia na deni kubwa kwa wakazi wa kata ya Ubagwe na wilaya ya Kahama kwa ujumla ya kuhakikisha kwamba inawaondolea kero mbalimbali ambazo iliahidi kuzifanyia kazi na kwamba moja ya vipaumbele vya serikali ya CCM kwa hivi sasa ni kilimo, afya, elimu na upatikanaji wa maji safi na salama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post