CCM noumaaaa!!!! YAWANYAKUA WALIOJIUZULU CHADEMA SHINYANGA,NAPE AWAPOKEA MADIWANI HAO WA CHADEMAShamra shamra baada ya waliokuwa nmadiwani wa Chadema kuonekana katika eneo la mkutano wa CCM mjini Shinyanga
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga mheshimiwa Gulam Hafiz Mukadam akishikana mkono na aliyekuwa diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga bwana Sebastian Peter Mzuka maarufu kama Obama wa Ngokolo muda muchache baada ya kuwasili katika viwanja vya mahakama ya Mwanzo Nguzo 8 mjini Shinyanga katika mkutano wa katibu wa siasa na uenezi wa ccm taifa Nape Nnauye ,mkutano ambao wananchi wameouona kama ulikuwa na nia ya kuwapokea viongozi wa chadema Sebastiani Peter na Zacharia Mfuko wa kata ya Masekelo ambao kwa pamoja jana walifanya maamuzi ya kujivua udiwani wa kupitia tiketi ya CHADEMA.
Waliokuwa madiwani wa CHADEMA,kulia ni Sebastian Peter,aliyekuwa diwani wa Ngokolo katikati ni Nape Nnauye na kulia ni Zacharia Mfuko aliyekuwa diwani wa Chadema kata ya Masekelo wakiwa juu ya jukwaa kabla ya kuvua kombati zao na kurudisha kadi zao kisha kujiunga na CCM mbele ya Nape Nnauye jioni ya leo mjini Shinyanga

Sebastian Peter akikabidhi kadi ya CHADEMA kwa Nape Nnauye
Awali wakati wa mkutano wa hadhara wa Chama cha mapinduzi CCM jioni ya leo,Katibu wa siasa na uenezi CCM taifa Nape Nnauye akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Shinyanga katika viwanja vya mahakama ya mwanzo eneo la Nguzo Nane mjini Shinyanga.Kushoto ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini,ambaye pia ni naibu waziri wa madini Stephen Masele.
Aliyekuwa diwani wa Chadema Zacharia Mfuko juu ya jukwaa la CCM kama unavyoona amevaa kofia na skafu ya Chama tawala.
 Zacharia Mfuko akizungumza katika mkutano wa hadhara na kutangaza nia ya kuhamia CCM
Aliyekuwa diwani wa Chadema katika kata ya Ngokolo Sebastian Peter akizungumza katika mkutano wa CCM leo ambapo alisema ameamua kujiunga/kurudi nyumbani kwa hiari yake bila kushinikizwa na mtu yeyote na kukanusha habari zilizotapakaa mtaani kuwa yeye pamoja na mwenzake Zacharia Mfuko wamehongwa shilingi milioni 15 ili wahamie CCM.
 
Sebastian Peter akivua kombati na kuvua nguo za CCM

Viongozi mbalimbali akiwemo meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafiz Mukadam (wa kwanza kulia) na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga bi Anna rose Nyamubi pamoja viongozi wengine akiwemo katibu wa ccm mkoa na katibu wa siasa na uenezi CCM wakifuatilia  kwa umakini maneno ya wanachama wawili wapya Chama tawala CCM
Kombati za CHADEMA walizokuja wakiwa wamevaa wazivua na kuzichoma moto hadharani kama unavyoona zikiteketea kwa moto


Ndani ya gari la CCM Sebastian Peter na Zacharia Mfuko wakiondoka eneo la mkutano wameshavaa nguo za CCM kama unavyoona

Hili ndiyo gari waliyoondoka nayo wanachama hao wapya wa CCM katika eneo la mkutano mjini Shinyanga huku maswali mengi yakiendelea kubaki kwenye vichwa vya wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuhusu maamuzi hayo waliyofikia kwa kukiona chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA si kitu tena pamoja na kwamba walikisifia kwa maneno matamu mwaka 2010 na kufanikiwa kupata kiti cha udiwani,lakini pia wengine kujiuliza kwanini wafanye vile wakati walikuwa wamebakiza muda mfupi tu kumaliza kazi waliyokuwa wamepewa na wapiga kura wao!!!

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post