Baada ya ushindi mnono !!! CCM YAWASHUKURU WANANCHI KWA KUIPA USHINDI UCHAGUZI WA MADIWANI WA JANA

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza  na waandishi wa habari leo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewashukuru Watanzania kwa kukiamini na kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika jana katika kata 27 na CCM kushinda kata 23. 

Akitoa shukrani hizo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema leo kwamba siri ya CCM kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia wananchi na kwamba, kushindwa kwa chama hicho ni ushahidi kwamba hakikubaliki na Watanzania wamewathibitishia kwamba hawajazoea vurugu.

Nape alisema CCM inaahidi kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa amani na utulivu kwa kuwa ina uzoefu wa kufanya siasa kistaarabu na ndio siri ya kukubalika kwa wananchi.

Akizungumzia kushindwa kwa CHADEMA alisema wamehukumiwa kutokana na vurugu na kupiga watu kwenye kampeni za uchaguzi na ndio maana wametumia gharama kubwa na helkopta tatu na kuambulia kata tatu.

"CHADEMA wamevuna walichopanda Watanzania hawapendi vurugu, wamezoea amani na utulivu sasa wamewaadhibu kwa kuwanyima kura na huo ni ushahidi kwamba Watanzania hawakiamini," alisema.

Katika uchaguzi huo CCM  ilishinda katika kata 23 za Kibindu na Magomeni (Pwani), Kiwalala na Namikage (Lindi), Ubwage (Shinyanga), Ibumu na  Nduli (Iringa), Kiomoni na Mtae (Tanga), Nyasura(Mara), Malindo, Santillya (Mbeya), Partimbo(Arusha, Mkwiti (Mtwara), Tungi na Ludewa (Morogoro) na Mrijo (Dodoma).
Credit-eddy blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post