 |
Ni katika kata ya Ndembezi katika mjini Shinyanga ambapo mwandishi wa Malunde1 Blog alikuta shughuli ya uchimbaji wa mitaro katika eneo la Oxfam jirani kabisa na Radio Faraja na kuelezwa kuwa kuna mtaro unachimbwa kutoka eneo la Oxfam hadi Barabara ya Kalogo mjini Shinyanga ikiwa ni moja ya njia ya kupambana na mafuriko hasa katika kipindi hiki cha mvua kwani eneo hilo hukusanya maji ya mitaa miwili ya kata hiyo yaani Mtaa wa Mbuyuni na mtaa wa Mabambasi yote ikiwa ni mitaa iliyopo katika kata ya Ndembezi |
 |
Kufuatia hali hiyo mwandishi wa Malunde1 Blog aliongea na Diwani wa kata hiyo ya Ndembezi ambaye pia ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga ndugu David Nkulila ambapo alisema suala la ujenzi wa mitaro na kalavati miongoni mwa vipaumbele vya manispaa ya Shinyanga.Aliongeza kuwa kufuatia ujenzi huo wa mtaro utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuwaepusha wananchi wa maeneo hayo kukumbwa na mafuriko lakini pia kitendo cha ujenzi wa mitaro ni moja ya hatua ya maendeleo katika kata hiyo |
 |
Hiyo ndiyo hali halisi ya shughuli inayoendelea katika kata ya Ndembezi mjini Shinyanga,uchimbaji wa mitaro unaendelea ambapo mitaro hiyo inajengwa kwa mawe na zege |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527
Post a Comment