Unyama tena Geita!!!! MTOTO ATOBOLEWA TUMBO BAADA YA KUTUHUMIWA KUFICHA MAFUTA YA KUJIPAKA NA BABA YAKE WA KAMBO

Mtoto Amosi Julius Mayila(12) aliyejeruhiwa na baba wa kambo baada ya kutuhumiwa kuficha mafuta ya kujipaka na hadi sasa kijana huyo akiwa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita kwa ajili ya matibabu

Mtoto mmoja wa mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa kijiji cha Mwendakulima kata ya Butengo na tarafa ya Buseresere wilayani Chato mkonai Geita amejeruhiwa kwa kutobolewa tumboni na kitu chenye ncha kali na Baba yake wa kambo aliyefahamika kwa jina la Sesa Charles.

Tukio hilo limetokea Januari 19 mwaka huu kijijini hapo ambapo kijana huyo Amosi Julius Mayila(12) alipata mkasa huo kutoka kwa baba huyo mara baada ya kutuhumiwa kuficha mafuta ya kujipaka na hadi sasa kijana huyo amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita kwa matibabu zaidi.

Akisimulia kuhusu tukio hilo  mama wa mtoto anayemuuguza katika hospitali ya wilaya ya Geita wodi namba 8 Bi Anastazia Sanyenge(39) alisema kuwa yeye alikuwa ameenda kwenye sherehe ya harusi kijiji jirani cha Bumba siku ya ijumaa na wake wenzake 2 kwani mme wao ana wanawake 3 na ndipo siku ya jumapili aliporudi nyumbani na kukuta watu wengi na mmewe akiwa amekimbia.

Naye jirani yake aliyemsaidia kumpeleka hospitalini Bw Benedict Faustine alisema kuwa akiwa nyumbani alifuatwa na watoto wakimwambia mwenzao ameanguka mtini na kuangukia kisiki lakini alipoenda nyumbani akakuta kijana amepigwa na utumbo umetoka nje na wakaanza kutoa msaada wa kumpeleka hospitali alipolazwa hadi sasa hivi.

Kwa upande wa mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Geita Bw Adamu Sijaona alisema kuwa walimpokea motto huyo mnamo saa 7 siku hiyo usiku akiwa na hali mbaya sana utumbo ukiwa nje na kulazimika madaktari watatu wamfanyie upasuaji na kumshona hali na kwamba hali yake sasa inaendelea vizuri

Kamanda wa polisi mkoani hapa Kamishina msaidizi mwandamizi Bw, Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio na kueleza kusikitishwa na kitendo cha Baba huyo wa kambo kutenda kitendo cha kinyama namna hiyo katika jamii.

Kamanda amesema  hadi sasa hivi mtuhumiwa anatafutwa na jeshi la polisi popote alipo ili sheria ichukue mkondo wake kwani amekimbia baada ya kutenda unyama huo.

Naye katibu wa Kituo cha kutetea haki za Binadamu wilayani hapa Bw Elineema Charles aliyeenda hospitali kumjulia hali kijana huyo amelaani sana kitendo hiki kilichofanywa na mtu mzima mwenye akili timamu na kuongeza kuwa adhabu kwa watoto zipo zinafahamika na si unyama wa aina .

Ameviomba vyombo vya sheria kwa kushirikiana na kamanda wa polisi huyo wa Geita kwani anaamini atapatikana tuili sheria ichukue mkondo wake.

Na Valence Robert- Geita


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post