SHINYANGA WAZINDUA BODI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA

Mapema leo akizungumza katika uzinduzi wa bodi ya hospitali ya rufaa ya mkoa katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Shinyanga kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ramadhani Kabala ambapo alisema kuundwa kwa bodi hiyo ni kuleta mabadiliko katika huduma za hospitali ikiwa ni sehemu ya mabadiliko endelevu katika sekta ya afya chini ya mkakati wa pili.
 Dkt Kabala alisema lengo la mkakati huo ni kuimarisha uwezo wa hospitali za mkoa na kanda ili ziweze kutoa huduma bora za rufaa  itolewayo na wizara ya afya na ustawi wa jamii chini ya usimamizi wa bodi zenye uwakilishi wa jamii.

Watu mbalimbali waliohudhuria shughuli ya uzinduzi wa bodi hiyo wakisikiliza hotuba ya Dkt Kabala kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa wa Shinyang aliyekuwa mgeni rasmi,ambapo Dkt Kabala alisema  miongoni  maeneo ambayo yanayohitaji mabadiliko ni pamoja na kutotosheleza kwa wataalam mbalimbali katika hospitali kutokana na hospitali nyingi kukosa uwezo wa kutoa huduma zote za matibabu kwa kiasi kinachostahili kutolewa.
 Eneo jingine ni kukosekana kwa motisha,kushuka ari na mtazamo mbaya watoa huduma kwa wagonjwa kushuka kwa kiwango na kukosekana kwa udhibiti wa ubora wa huduma,uchakavu wa vifaa,vifaa tiba,miundombinu na magari

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza wakati akizindua bodi ya hospitali ya rufaa ya mkoa katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Shinyanga,ambapo alisema endapo suala la afya likipewa kipaumbele litasaidia katika kuondoa umaskini katika jamii kwani wananchi watajihusisha na shughuli za maendeleo kutokana na kwamba afya zao ni nzuri. 
Alisema anaamini kabisa kwamba bodi hiyo inayoundwa na wajumbe 17 itakuwa mwakilishi mzuri wa wananchi na kutoa rai kwao wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi,na kwamba wahakikishe wanafanya vikao mara kwa mara yaani kila baada ya miezi mitatu na wafanye kazi kwa uhakika

Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa bodi hiyo


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post