
Katika hali isiyo ya kawaida maiti ya mtoto mchanga imekutwa imetupwa katika
eneo la kuhifadhia taka "jalala" huko Mbagala Nzasa A, maiti ya kichanga
hicho ilikutwa ikiwa inatoa harufu huku mwili wake ukiwa umeharibika
vibaya kutokana na kuliwa na wadudu.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema maiti ya kichanga hicho ilikuwa imefungwa katika kanga yenye rangi nyeupe na bluu huku idadi kubwa
ya Nzi ikiwa inazonga maiti hiyo ikiwa imeharibika vibaya sana.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo akiongea kwa masikitiko makubwa alidai
kuwa siyo mara ya kwanza tukio hilo kutokea katika eneo hilo kwani
miaka miwili nyuma tukio kama hili liliwahi kutokea na mhusika
alikamatwa baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na polisi wakisaidiana
na raia wema.
Naye
mjumbe wa eneo hilo Bwana Saidi Kitambulio alishangazwa na kutokea kwa
tukio hilo la kustaajabisha na kulaani vikali na kusema kuwa wametoa taarifa kituo cha polisi cha jirani ambapo jeshi la polisi
litaendelea na utaratibu wake wa kawaida wa kumtafuta muhalifu
aliyemtupa mtoto huyo eneo hilo.
Post a Comment