Taarifa zilitufikia, zinasema
kuwa, mfanyabiashara wa simu eneo la Ilomba Jijini Mbeya, amepigwa
risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo,
alipokuwa akielekea nyumbani kwake.
Imeelezwa kuwa alitoka dukani kwake
ambako anauza simu akielekea nyumbani kwake eneo la
Isyesye Nanenane, ndipo alipovamiwa na watu hao kisha kumpiga risasi ya
mguuni na kumpora fedha na gari lake na sasa amelezwa hospitali ya rufaa
ya Mbeya kwa ajili ya matibabu.
Jeshi la polisi mkoani Mbeya, linaendelea kuwasaka watu hao.
credit-kalulunga blog
Social Plugin