Majanga!!!! JAMAA APANDA JUU YA MNARA WA SIMU ,AGOMA KUSHUKA MPAKA RAIS KIKWETE AJE ASIKILIZE KERO ZAKE...!!!

Mwanaume mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja amepanda juu ya mnara wa kampuni ya simu za
mkononi ya Vodacom uliopo Ubungo katika eneo la ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  jijini Dar es Salaam na kutaka kujirusha.

Katikakati jamaa akiwa juu ya mnara
Wananchi wakimwangalia jamaa akiwa juu ya mnara wa simu

Wakazi wa Dar es salaam waliofika eneo la tukio

Jamaa akizungumza na wanahabari katika eneo la tukio baada ya kushushwa ,ambapo aliwatuhumu askari polisi kwa kuwabambikiza kesi wananchi.

Mwanaume huyo amedai alitaka kufanya hivyo ili kufikisha ujumbe kwa Rais Jakaya Kikwete baada ya kudai kufungwa miaka sita jela kwa kubambikiziwa kesi na  polisi.

Mwanzoni alikataa katakata kushuka kutoka katika mnara huo akidai mpaka Rais Kikwete afike eneo hilo aweze kumweleza kero yake hiyo japo wanausalama walifanikiwa kutumia mbinu zao kumshawishi asijirushe na kufanikiwa kushuka naye.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post