Inatisha!!! JAMAA AKUTWA AMEJINYONGA BAFUNI,KAMA NI MUOGA USIANGALIE PICHA ZINATISHA,TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZO


Matukio ya kutisha yamezidi kuchukua sura mpya nchini Brazil baada ya mtu mmoja asiyefahamika kukutwa akiwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha baada ya mwili wake kukutwa akiwa amenyongwa bafuni.Mtu huyo inasemekana amekaa kwa muda mrefu akiwa amefariki bila majirani zake pamoja na ndugu zake kujua kuwa amekufa kwani mwili wake ulikutwa umeharibika sana.

Haijaweza kufahamika mara moja kuwa aidha mtu huyo alinyongwa au yeye mwenyewe aliamua kujinyonga akiwa anaoga bafuni.Wataalam wa jeshi la polisi walieleza kuwa wanashuku kuwa huenda mtu huyo alinyongwa kwa sababu si hali ya kawaida mtu kujinyonga akiwa anaoga huku amevua nguo,ushahidi wa kimazingira unaonyesha kuwa mtu huyo alikuja kudhuriwa na watu wasiofahamika wakati alipokuwa akioga bafuni kwake.

Nao majirani wa marehemu huyo walisema kuwa hawakuwahi kuona wala kuhisi uwepo wa jirani yao huyo mpaka baada ya muda mrefu kusikia harufu kali ikitoka nyumbani kwa mtu huyo,ndipo walipoamua kutoa taarifa kituo cha polisi kilichopo karibu yao ili hatua zaidi za kisheria zichukuliwe ndipo polisi walipowasili kwenye nyumba hiyo na kumkuta mtu huyo akiwa ameoza kabisa mwili mzima.

Credit- mamboyawalimwengu.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post